Marie-Roger Biloa
Marie-Roger Biloa ni raia wa nchi ya Kamerun anayejishighulisha na uhariri wa magazeti, uendeshaji wa vipindi vya televisheni, uandishi wa Habari, utengenezaji wa filamu pia ni mwenyekiti wa shughuli mbalimbali za kijamii. Anaishi katika nchi ya Ufaransa ambapo anaendesha kipindi cha televisheni. Akiwa huko alipewa tuzo ya kutambua mchango wake katika sanaa na uandishi. [1] Katika kazi zake za uandishi, pia aipokea tuzo ya Percy Qoboza. Bi Biloa pia anamiliki mtandao uitwao Africa-international.info.
Maisha ya Mwanzo
[hariri | hariri chanzo]Biloa ni binti wa Germain Tsala Mekongo, ambaye katika mwaka 1957 alikuwa Katibu wa Jimbo la Utumishi wa Umma; akitumikia cheo hicho kama mtu wa kwanza kutunukiwa cheo hicho. Alienda katika Chuo kikuu cha Paris-IV Universit], ambapo alifuzu katika masomo ya Kijerumani.[2]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Katika mwaka 1991, Biloa alikuwa mhariri wa jarida la Africa International, ambalo lilianzishwa mwakaa 1958; wakati Biloa anajiunga nalo, jarida hilo lilikuwa likiandika masuala ya siasa, habari za kiuchumi na asili ya Mwafrika.[1]
Baadaye, Biloa alijiunga na jarida la controversial pan-African themed Jeune Afrique, ambalo hapo kabla lilikuwa limefungiwa katika nchi kadhaa za kiarabu zilizoko upande wa kaskazini mwa Afrika [3]
Katika mwaka 1997, Biloa alipewa tuzo ya heshima kama mwandishi bora wa mwaka huo na shirika la Kimarekani liitwalo the National Association of Black Journalists, akipokea tuzo kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Marekani kwa wakati huo Bill Clinton.[1]
Katika mwaka 2001, Biloa alipewa jina la mwanamke wa ubora na shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na kulinda amani duniani liitwalo Unesco.[1]
Ufunguzi wa kituo cha Televisheni
[hariri | hariri chanzo]Bi. Biloa, katika mwezi wa October 15, 2018, ilitangazwa kwamba atafungua kituo kipya cha televisheni kikitambulika kwa jina la MRB TV (isichanganywe na MRB Productions, ambayo ni kampuni ya uzalishaji wa filamu ya Marekani), ambacho kilirusHa matangazo yake kupitia satelaiti.
Taarifa binafsi
[hariri | hariri chanzo]Anaongea lugha mbalimbali vizuri ikiwemo Kiingereza, Kihispania, Kifaransa na Kijerumani. Biloa anaishi katika miji ya Paris, Berlin na Yaounde, Cameroon.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "Marie-Roger Biloa élevée en France au rang de chevalier de l'Ordre, des arts et des lettres". Aprili 9, 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Denise Epoté Durand, Marie Roger Biloa et elizabeth Tchoungui : les amazones du PAF". Oktoba 6, 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Jeter, James Phillip; Rampal, Kuldip R.; Cambridge, Vibert C.; Pratt, Cornelius B. (Oktoba 30, 1996). "International Afro Mass Media: A Reference Guide". Greenwood Publishing Group – kutoka Google Books.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Marie-Roger Biloa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |