Nenda kwa yaliyomo

Maria W. Stewart

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maria W. Stewart
Amezaliwa Maria W. Stewart
1803 Desemba 17
Marekani
Kazi yake Mwandi wa habari
Cheo mwalimu

Maria W. Stewart (née Miller ) (1803 - Desemba 17, 1879) alikuwa mzaliwa wa Marekani na Afrika ambaye alikua mwalimu, mwandishi wa habari, mhadhiri, mteteaji wa haki za wanawake na mwanaharakati. Alikua mwanamke wa kwanza wa kimarekani kuzungumza na hadhira mchanganyiko ya wanaume na wanawake, weupe na weusi, pia alikuwa mwanamke wa kwanza Mwafrika-Mmarekani kufanya mihadhara ya umma, na vile vile kuongea juu ya haki za wanawake na kutoa hotuba kwa uuma kupambana na utumwa. [1] Liberator (gazeti la kupambana na utumwa) | Mkombozi ni moja ya magazeti aliyo yahudumia.aliwahi kuchapisha vijikaratasi viwili vilivyosema: Dini na Kanuni safi za Maadili, Msingi wa Hakika Ambayo Tunapaswa Kujenga (ambayo ilitetea utumwa wa mtu mweusi) mnamo mwaka 1831, na tafakari nyingine ya kidini, Mnamo Februari 1833, alihutubia Boston's African Masonic Lodge. Madai yake yalikua wanaume weusi walikosa "shahuku na ujasiri wa lazima" ilisababisha ghasia kati ya mkutano, na Stewart aliamua kustaafu kutoa hotuba kwenye mikutano. Miezi saba baadaye, alitoa hotuba ya kuaga kwenye chumba cha shule katika Nyumba ya Mkutano wa Afrika ("Kanisa la Paul"). Baada ya hapo, alihamia New York City, kisha Baltimore, na mwishowe Washington, DC, ambapo alifanya kazi kama mwalimu, na kisha mkuu wa shule.Alifariki kwenye Hospitali ya Freedmen.

Maisha ya mapema

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa Maria Miller, mtoto wa wazazi wa Kiafrika na Marekani huko Hartford, Connecticut. Mnamo mwaka ï1806, akiwa na umri wa miaka mitatu alipoteza wazazi wote wawili na akapelekwa kuishi na waziri na familia yake. Aliendelea kuwa mtumishi katika nyumba hiyo hadi alipokuwa na miaka 15, bila kupata elimu yoyote rasmi. Kati ya umri wa miaka 15 hadi 20, Maria alihudhuria Shule ya Sabato kabla ya ibada ya Jumapili na kukuza ushirika wa maisha yake na kazi ya dini.[2] Mnamo Agosti 10, mnamo mwaka 1826, Maria Miller aliolewa na James W. Stewart, wakala wa usafirishaji, mbele ya Mchungaji Thomas Paul, mchungaji wa Nyumba ya Mkutano wa Afrika, huko Boston, Massachusetts. Hakuchukua tu jina lake la mwisho bali pia na jina la kati la mumewe.[3]Ndoa yao ilidumu kwa miaka mitatu tu na hawakuweza kupata watoto; James Stewart alifariki mnamo mwaka 1829. Wasimamizi wa mali yake walimnyima Maria kama mjane wake urithi wowote. Wakati huu ulimchochea Stewart kuanza kufikiria juu ya haki za wanawake na ukosefu wa haki waliokabiliana nao.[4]Walakini, James alikuwa amehudumu katika Vita ya mwaka 1812 na mwishowe sheria ilipitishwa inayowaruhusu wajane kupata pensheni za waume zao. [5]

Kifo na urithi

[hariri | hariri chanzo]

Stewart alifariki katika Hospitali ya Freedmen mnamo Desemba 17, 1879. Alizikwa uko Graceland Cemetery, wilaya ambayo mazishi hufanyika.[6] Kalenda ya watakatifu (Kanisa la Maaskofu uko marekani huwa linafanya kumbukizi ya Maria Stewart kila mwaka, pamoja na William Lloyd Garrison mnamo Disemba 17.

Stewart amejumuishwa katika maandiko ya dina na wanaharakati kama vile Daughters of Africa: an International Anthology of Words and Writings by Women of African Descent , iliyohaririwa na Margaret Busby (1992),[7] jina ambalo lilichochewa na tangazo la Stewart la mwaka1831,[8]

  1. Maggie MacLean,"Maria Stewart", History of American Women, Abolitionists.
  2. America's First Black Woman Political Writer, edited by Marilyn Richardson.
  3. "Maria Stewart, Abolitionist, Public Speaker, Writer" Archived 25 Februari 2017 at the Wayback Machine., Women's History, About.com.
  4. Dionne, Evette (2020). Lifting as we climb : Black women's battle for the ballot box. New York. ISBN 978-0-451-48154-2. OCLC 1099569335.{{cite book}}: CS1 maint: location missing publisher (link)
  5. Ashira Adwoa, "Maria W. Stewart" Archived 5 Aprili 2012 at the Wayback Machine., African American (December 13, 2010).
  6. "Maria W Stewart: District of Columbia Deaths and Burials, 1840-1964", FamilySearch, accessed June 4, 2012.
  7. Margaret Busby (ed.), Daughters of Africa: An International Anthology of Words and Writings by Women of African Descent, London: Jonathan Cape/New York: Pantheon, 1992, "Introduction", p. xxix.
  8. Herb Boyd, "Maria W. Stewart, essayist, teacher and abolitionist", New York Amsterdam News, April 25, 2019.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maria W. Stewart kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.