Nenda kwa yaliyomo

Margareta Trnková-Hanne

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Margareta Trnková-Hanne (anajulikana pia kama Margareta Hanne; amezaliwa 17 Novemba 1976) ni mwanamichezo wa kike wa zamani wa riadha na tenisi kutoka Jamhuri ya Ucheki ambaye ni kiziwi.[1] Ameiwakilisha Jamhuri ya Ucheki katika michezo ya viziwi upande wa tenisi na riadha.[2]

Margareta Hanne alishiriki katika Michezo ya Majira ya Joto ya Viziwi mwaka 1993, 1997, 2001, 2005, na 2009.[3]

Pia alishinda medali nne za dhahabu katika michezo ya viziwi upande wa wanawake kwa 100m na 200m. [4][5][6] Pia aliteuliwa kwa tuzo ya Mwanamichezo Kiziwi wa Mwaka ya ICSD mwaka 2001 na 2005, hasa kwa mafanikio yake katika Michezo ya Viziwi ya 2001 na 2005.[7]

  1. "Margareta Trnkova-Hanne". Deaflympics. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-01-03. Iliwekwa mnamo 2018-01-03.
  2. "Trnková-Hanne Margareta". csns-atletika.wz.cz. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-01-04. Iliwekwa mnamo 2018-01-03.
  3. "SKN Brno". sknbrno.net. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-01-04. Iliwekwa mnamo 2018-01-03.
  4. "Czech athletes return triumphant from Melbourne Deaf Olympics". 
  5. "Handicapovaným kraluje Maléřová", Aktuálně.cz, 2006-02-07. (cs) 
  6. "Melbourne 2005 Deaflympic Games - Athletics". SportsTG. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-01-04. Iliwekwa mnamo 2018-01-03.
  7. "News". Deaflympics. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-07. Iliwekwa mnamo 2018-01-03.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]