Marathoni ya Boston
Mandhari
Marathoni ya Boston ni mbio ya Marathoni maarufu ambayo inaendeshwa kila mwezi wa Aprili katika mji wa Boston nchini Marekani. Umbali wa mbio ni maili 24.5 ambayo ni sawa na km 39.4.
Ili kupata kibali cha kushiriki, mkimbiaji anahitaji kuonyesha kuwa amemaliza mbio tofauti ya Marathoni kwa muda fulani. Muda huo unaohitajika ni tofauti kulingana na umri wa mkimbiaji.
Idadi ndogo ya wakimbiaji inakubaliwa kila mwaka wasiotimiza masharti hayo, wakishiriki kwa kusudi la kukusanya pesa kwa madhumuni za kijamii.
Mashambulio ya 2013
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa Marathoni ya Boston ya mwaka 2013 yalitokea mashambulio ya kigaidi. Milipuko miwili ilitokea karibu na mstari wa kumaliza iliyoua watu watatu na kujeruhi watazamaji 183. [1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Explosions rock Boston Marathon, several injured", CNN, April 15, 2013. Retrieved on April 15, 2013.
Tovuti nyingine
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti rasmi Archived 19 Septemba 2008 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Marathoni ya Boston kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |