Malkia (sataranji)
Mandhari
Malkia ni kete ya mchezo wa sataranji ambayo inasimama karibu na shaha mwanzoni mwa mchezo. Malkia hukaa kwenye mraba d1 kwa upande mweupe na mraba d8 kwa upande mweusi. Inaweza kusogea idadi yoyote ya miraba isiyokaliwa kwa mshazari, wima, au mlalo . Wakati wa kurekodi michezo, inatajwa kwa kifupi cha "Q".
Malkia hutazamiwa kuwa kete yenye uwezo mkubwa kushinda zote kwenye sataranji.
Mwendo wa malkia
[hariri | hariri chanzo]Malkia anaweza kusogea kama sataranja (bishop) na ngome (rook). Kila mchezaji huanza na malkia mmoja. Mchezaji anaweza kubadilisha kitunda kuwa malkia wakati kinafika mstari wa mwisho wa ubao.