Nenda kwa yaliyomo

Malindi Elmore

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Malindi Elmore mnamo 2010 Dave Reed Spring Classic 5K
Malindi Elmore mnamo 2010 Dave Reed Spring Classic 5K

Malindi Elmore (alizaliwa Kelowna, British Kolumbia, Machi 13, 1980) [1] ni mwanariadha mwenye asili ya Kanada ambaye ni bingwa wa mbio za kati[2][3]. Mnamo Januari 19, 2020 alishikilia rekodi ya marathoni ya nchini kanada kwa kukimbia ndani ya dakika 2:24:50.[4]

Ni mshindi wa mara tano mfululizo wa All-American kutoka chuo kikuu cha Stanford na kushikilia rekodi ya shule ya kukimbia umbali wa mita 800 na mita 1500. Aliiwakilisha kanada mwaka 2004 katika Michezo ya Olimpiki ya majira ya joto,lakini alishindwa kupita kwenye nusu fainali.

Alishinda katika mashindano ya Vancouver Sun Run ya mwaka 2010 kwa kutumia muda wa dakika 33:06 kwa kilomita zaidi ya 10.[5]

Alifanikiwa kuiwakilisha kanada katika Michezo ya Olimpiki ya majira ya joto ya 2020 mnamo Juni 2021[6] na kumaliza nafasi ya tisa katika marathoni kwa upande wa wanawake.[7]

  1. "Malindi Elmore Bio, Stats, and Results | Olympics at Sports-Reference.com". web.archive.org. 2020-04-18. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-04-18. Iliwekwa mnamo 2021-09-28.
  2. "Malindi ELMORE | Profile | World Athletics". www.worldathletics.org. Iliwekwa mnamo 2021-09-28.
  3. "Malindi Elmore". Team Canada - Official Olympic Team Website (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-09-28.
  4. "Malindi Elmore shatters Canadian marathon record in 2:24:50". Canadian Running Magazine (kwa American English). 2020-01-19. Iliwekwa mnamo 2021-09-28.
  5. "Malindi Elmore, Willy Kimosop all set to defend titles, as CRS2011 opens at Harry's Spring Run Off Vancouver 8K. | Scotiabank Toronto Waterfront Marathon". web.archive.org. 2016-05-13. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-05-13. Iliwekwa mnamo 2021-09-28.
  6. "Athletics Canada announces Olympic marathon teams". Canadian Running Magazine (kwa American English). 2021-06-04. Iliwekwa mnamo 2021-09-28.
  7. Hill, Andrea (2021-08-07), "Olympic redemption 17 years in the making; Malindi Elmore thrilled with top-10 marathon result", National Post (kwa Kiingereza), iliwekwa mnamo 2021-09-28
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Malindi Elmore kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.