Majadiliano ya mtumiaji:Sarahwllms

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyara za kufuli[hariri chanzo]

Kufuli[1] ni kifaa ambacho kina matumuzi mengi, kama vile kuhifadhi mali ama stakabadhi muhimu, kufungia mnyama ama mtu mhalifu mahali fulani, kuzuia kupotea kwa mali, na mambo mengineyo. Huo ukiwa mtazamo, ni ishara kwamba kufuli ni za aina tofauti, kulingana na mambo kama;

  • Inatumika wapi hasa
  • Kiwango cha usalama [2]
  • Thamani ya mali inayolindwa

Nyara ya kufuli ni mkwaju wa chuma ambao hutumika kufungia kufuli kwenye kifunguo. Hizi pia hutofautiana katika ubunifu kulingana na matumizi ya kufuli.

Aina za nyara za kufuli[hariri chanzo]

Nyara ndefu[hariri chanzo]

Kufuli hizi huwa na nyara ndefu zaidi kuliko zote na hutumika kwenye vifungo kubwa kama milango, sanduku, na nyororo. Huwa rahisi kufunga lakini mwanya huo mkubwa huwa rahisi kukata, kugonga kwa nyundo ama kuvunja kwa claw bar[3]

Nyara iliyozibwa[hariri chanzo]

Katika kufuli hizi, mwili wa kufuli huwa na mabega marefu ili yafiche nyara kufuli inapofungwa. Nyara yenyewe huwa fupi na hutumika mahali ambapo usalama wa kiwango cha juu unahitajika, kama vile benki, kufuli za sanduku la hifadhi, ulinzi, na kadhalika.

Nyara nusu wazi[hariri chanzo]

Nyara hizi huwa fupi na zimefichwa kidogo na mabega ya kufuli. Hutumika mahali panapohitaji usalama wa kimo cha kati kwa sababu si rahisi kukata ama kuvunja kama nyara ndefu, ingawaje si imara kama nyara iliyozibwa. Kufuli hii yatumika sana nyumbani.

Nyara songefu[hariri chanzo]

Katika kufuli hii, waweza kusongesha nyara ikawa ndefu, yenye urefu wa kimo ama fupi kulingana na mahitaji yako. Kufuli ikiwa hivo, urahisi wa kuikata ama kuvunja kwa kiwango kikubwa utategemea urefu wa nyara uliotumika.

Viungo vya nje[hariri chanzo]

  • Best locks for storage units[1]
  1. [ https://sw.wikipedia.org/wiki/Kufuli ] Kufuli
  2. [2]usalama
  3. [3]claw bar