Majadiliano ya mtumiaji:Ramadhani Msangi

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Utamaduni wa Mtanzania[hariri chanzo]

--Ramadhani Msangi 07:38, 25 Novemba 2005 (UTC)Licha ya kuwa dunia hivi sasa imekuwa kama kijiji kimoja, kutokana na maendeleo ya hali ya juu ambayo yamefikiwa katika nyanja ya Sayansi na Teknolojia, hali ambayo inawafanya Walimwengu kuchangamana katika tamaduni zao, bado upo umuhimu wa bara la Afrika, kama bara La Afrika, kuelewa fika na kuzitambua kwa utimilifu Tamaduni zao.[jibu]

Likiwa bado linakabiliwa na umasikini wa hali ya juu, huku pia likiwa bara pekee ambalo lina rasilimali zenye kuweza kushibisha njaa ya mahitaji ya malighafi mbalimbali za viwanda duniani, ni wazi kuwa ni kwa Waafrika wenyewe kujua, kutambua na kuziendeleza tamaduni zao ambapo wataweza kupiga hatua za haraka za kimaendeleo, kwakuwa wataondokana na utaratibu wa kuburuzwa na tamaduni za mataifa ya kimagharibi. Lakini je ni wangapi kati yetu ambao tunazikumbuka au kuzijua tamaduni zetu?. Utamaduni wa Mtanzania, kwa mfano, ni upi hasa?

Salaam, ndugu Ramadhani, ni vema kuwa na sauti kutoka Mbeya. Kuhusu swali lako: Wakati wowote utamaduni wa sehemu yoyote ni ule ulio njiani... utamaduni ni kama mto. Je, mto uko wapi??
Samahani lakini, kwa sababu hatuko kwenye blogu hapa ni karahana. Ombi: angalia makala ya Tukuyu usahihishe tafadhali. Ni muda mrefu sijafika Tukuyu hasa "taasisi" nimeandika zaidi kwa imani kuliko akili. --Kipala 15:42, 29 May 2006 (UTC)