Mtumiaji:Ramadhani Msangi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ramadhani Msangi ni mmoja wa wanablogu wakubwa kwa Kiswahili. Ramadhani ni mwandishi wa habari aliyekuwa na makazi yake katika mji mkuu wa Tanzania, Dodoma, wakati anaanza kublogu kabla ya kuhamishiwa kikazi [jijini Mbeya] toka Oktoba 2005, akiwa ni mwajiriwa wa kampuni ya [Business Times Ltd.].

Alidumu na Business Times Limited hadi mwaka 2008, ambako alijiunga na Mahakama ya Mwanzo ya Mwanjelwa kwa mafunzo ya sheria kwa vitendo, baada ya kuhitimu kozi ya sheria, ambako baada ya kumaliza mafunzo kwa njia ya vitendo, aliachana na mahakama hiyo na kupumzika kwa muda kabla ya kujiunga na Exim Bank Tanzania Limited, tawi la Mbeya, kama wakala wa mauzo, nafasi ambayo alidumu nayo hadi 2011.

Mwaka huo, alipandishwa na kuwa Afisa Masoko Mkuu katika tawi hilo, nafasi aliyodumu nayo hadi mwaka 2012, alipoachana na taasisi hiyo kwa ajili ya kujikita zaidi katika kuimarisha kampuni ya Jukwaa Huru, akishirikiana na waanzilishi wenza ambao ni Rashid Mkwinda na Fadhy Mtanga.

Kufikia mwaka 2014, Jukwaa Huru chini ya wakurugenzi wenza hao watatu, ilikuwa ikiendesha mtandao wa habari wa Jukwaa Huru Blog, majarida ya matangazo ya Advertising Mbeya na mengineyo kadhaa. Miongoni mwa matarajio ya kampuni hii kwa mwaka 2015, ni kuanzisha jarida jipya la simulizi nchini Tanzania, ambalo litalenga katika kuenzi lugha ya kiswahili, na likisambazwa katika sehemu/nchi mbalimbali zinazozungumza lugha ya kiswahili, zikiwemo zile za ughaibuni.