Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano ya mtumiaji:Mwakanosya

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Salam, Mwakanosya! Twamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi! Karibu tena hapa Uswahili - mahali ambapo umezoea kuwa. Haya, nimeona umeanzisha Lango la hisabati, lakini ndani yake hakuna kitu. Je, ungependa nikusaidie? Angalau tujue tulichofanya ni kitu gani! Ukiwa una swali lolote, basi uliza tu na utajibiwa! Nikiwa ninatokea Dar es Salaam, Tanzania, niite Muddyb au,--MwanaharakatiLonga 05:56, 27 Januari 2010 (UTC) [jibu]


Asante kwa salamu yako! Imenifurahisha kuona watu wengine wanaotumia Kiswahili kwenye intanet. Nimekaaa sana bila kupata nafasi ya kutumia Kiswahili Marekani. Yaani nilikuwa nimegundua makundi ya Kiswahili vyuoni, lakini sasa mimi ni mwanafanyakazi tu. Sasa, kuna muda fulani mpaka nitakapoanza shuleni tena, kwa hivyo nitapenda sana kutumia uwezo wangu wa kompyuta na hisabati kutengeneza kurasa za wikipedia. Bado sijapata information nzuri za kuanzisha kurasa hizo. Lakini nitaendelea na nitakuwa msaidizi wako.

--Mwakanosya 14:50, 27 Januari 2010 (CST)

Khe! Labda tu niseme pole! Wapo wengi wanaongea Kiswahili mtandaoni!!! Tena ni wengi ajabu.. Humu tuna Wajerumani wawili (Kipala na Oliver au Baba Tabita). Mwelisi mmoja na Mholanzi (ChriKo). Labda ningeseme tu kwa lugha yenu (you did not notice this Wikipedia before)! Laiti kama ungeijua hii, basi hata mshangao usingekuwepo! Basi ukipata nafasi na jambo la kuandika ukiwa nalo, basi twende kazi. Karibu tena...--MwanaharakatiLonga 07:31, 28 Januari 2010 (UTC)[jibu]