Majadiliano ya mtumiaji:72.95.250.97

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ndoto ya Amerika[hariri chanzo]

Ndoto ya Amerika ni kitabu cha watoto kilichoandikwa na Ken Walibora. Ken Walibora ni mwandishi maarufu wa Kenya. Amefanya kazi na kuandika zaidi ya vitabu ishirini. Ni mwandishi mzuri na ameshinda tuzo nyingi kwa kazi yake. Alishinda Tuzo ya Jomo Kenyatta Literature mara mbili kwa Ndoto ya Amerika mwaka wa 2003 na Kisasi Hapana mwaka wa 2009.


Wahusika[hariri chanzo]

  • Isaya Yano
  • Mama Isaya
  • Madoa
  • Mzee Zakayo Wekesa
  • Rock Mwamba

Utangulizi[hariri chanzo]

Kitabu hiki kinafuata maisha ya Isaya Yano. Isaya ndiye mhusika mkuu wa kitabu. Kitabu hicho pia kinaonyesha maisha ya rafiki mkubwa wa Isaya, Madoa. Mahali pa hadithi ni nchini Kenya. Isaya anaishi Sangura katika tarafa ya Cherangani, Wilayani Trans-Nzoia. Isaya na Madoa wote ni wavulana maskini wa mashambani ambao wana mama wabaya. Wanachotaka kufanya ni kupumzika na kutofanya kazi yoyote. Hawataki kuwa wakulima, hawataki kwenda shule, hawataki kufanya chochote lakini wanataka kujifurahisha. Walifurahi tu wakati wa likizo, mapumziko, mashindano ya michezo au siku kuu za kitaifa kwa maana hawakuwa na masomo.


Hii ni picha ya Ken Walibora. Alizaliwa mwaka 1965 huko Baraki, Bungoma, Kenya


Maudhui[hariri chanzo]

  1. Katika Ndoto ya Amerika niliona kuna maudhui nyingi kama:
  2. Umaskini
  3. Chuki kwa nyumba yao
  4. Kutaka kuondoka/ Kutoroka
  5. Migogoro
  6. Ndoto
  7. Kifo
  8. Msitu

Migogoro katika kitabu hiki inaonekana katika sura mbili za kwanza. Mama Isaya ni mtu mkali sana. Anaonyesha hisia zake kupitia migogoro. Unaweza kuona maudhui hii wakati Isaya analia na Mama Isaya anampiga kwa sababu alilia. Mauduhi ya migogoro inaendelea wakati Isaya na Madoa wanakamatwa na polisi baadaye kwenye kitabu.

Kutoroka ni maudhui mkubwa pia. Tunaona Isaya na Madoa wanataka kutoroka makwao na kutoroka kenya. Isaya kutaka kuota kuhusu marekani ni kuweza kutoroka kiakili. Msitu kupitia kitabu hiki ni muhimu sana. Ni mahali salama kwa Isaya na Madoa kutoroka. Isaya na Madoa wanataka kuondoka nyumba na kuacha shule zao lakini Madoa pia anataka kuondoka Afrika. Madoa hata anasema kila mtu wana ndoto ya kuondoka na kwenda marekani

Ndoto ni muhimu sana katika kitabu hiki. Maudhui hii inatuonyesha jinsi mtu anavyopaswa kuwa na jinsi anavyopaswa kufikiri. Kuota Amerika kwenye kitabu ni kitu muhimu sana. Msomaji anajifunza kwamba kila mtu anakuwa na ndoto ya Amerika. Kuwa na ndoto hii inaonyesha kuwa unataka zaidi katika maisha yako. Muhimu hii huleta swali, je, ni lazima uondoke nyumbani kwako ili ufurahe maisha kweli?


* Hii ni picha la kitabu, Ndoto ya Amerika * Picha ya jalada la kitabu ni ya Isaya chini ya mganga * Alipotorokea msituni, analala chini ya mti na ana ndoto yake ya kwanza kuhusu Amerika



<https://www.goodreads.com/author/show/1268985.Ken_Walibora />

<https://www.the-star.co.ke/news/2020-04-15-ken-walibora-life-and-times-of-renowned-author/ />


Huu ni ukurasa wa majadiliano kwa mtumiaji asiyejulikana ambaye bado hajafungua akaunti, au ambaye haitumii. 

Kwa hivyo inatubidi kutumia anwani ya IP ya nambari ili kuwatambua. Anwani kama hiyo ya IP inaweza kushirikiwa na watumiaji kadhaa. Ikiwa wewe ni mtumiaji asiyejulikana na unahisi kuwa maoni yasiyo na maana yameelekezwa kwako, tafadhali fungua akaunti au ingia ili kuepuka kuchanganyikiwa kwa watumiaji katika siku za usoni na wengine wasiojulikana.