Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano ya Wikipedia:Site support

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Natoa shukrani zangu na pongezi sana kwa mradi huu. Natazamia kuuchangia niwezavyo katika siku za usoni ili kuuendeleza mbele. Itakuwa vyema kwa kweli kuona mradi huu ukichangiwa zaidi na zaidi pia katika sayansi na tekinolojia.

Ben Mwashote

Ndugu Ben, ni kweli kabisa. Ni furaha kubwa kuwa utajiunga na jumuiya hii. Karibu sana. ----ndesanjo, Agosti 29, 2006

Ndugu Ben, karibu tu uchangie! Wikipedia hii bado ni ndogo. Tumefikia makala 1000 lakini si kubwa. Bado kuna lugha zisizozungumzwa tena kama vile Kilatini au Kikornwall bado ziko mbele. Mimi naota ndoto kupata walimu wa vyuo au hata sekondari wanaowapa wanafunzi wao kazi ndogondogo ya kuandika makala mafupi kwa ajili ya wikipedia ya Kiswahili. Unaonaje? --Kipala 15:58, 29 Agosti 2006 (UTC)[jibu]

KISWAHILI CHA KENYA SIYO KISWAHILI HALISI

[hariri chanzo]

Tafadhali, naomba leo niongee, ninasikitika sana kuona mara kwa mara wakenya wanajifanya wanajua kiswahili, wakati hawajui kabisa, ila wanaharibu kamusi ya kiswahili. Kitu kikubwa cha kuelewa, ni kwamba, kiswahili si lugha ya kuiga tu, kama tunataka kukiendeleza kiswahili halisi, ni bora kukiongea chenyewe halisi kwa msimamo halisi, sio kiswahili kilichochujuka na kilichojaa mikamusi isiyoeleweka wa watu wanaojifunza. Mimi binafsi nilizaliwa na kiswahili toka utoto wangu, na mara nyingi nikitembelea Kenya huwa nashangaa kwanini wakenya wanasema wanajua kiswahili, wakati hata Warundi na Wakongoman wanawazidi mbali sana.

Nadhani, kosa kubwa wanalolifanya wakenya, ni kutoweka kiswahili kuwa lugha ya mawasiliano kwenye vyombo vya habari na elimu, ndio maana hawajui kabisa kiswahili, labda kidogo watu wa Mombasa, ila wengine wote, weupe kabisa kwa kiswahili. Naomba watu wanaoandika makala mbalimbali humu, wazingatie kiswahili halisi, hasa kile cha kitanzania, sio kiswahili mfu. Ijulikane moja kama wewe unajua kiswahili, basi changia, kama haujui kiswahili basi nenda shule kajifunze kuliko kutoa uozo wa lugha ukijifanya unajua. wenzio watakucheka. Asante.

Mtenga Dar es salaam, Tanzania.

Kiswahili cha Tanzania siyo halisi zaidi kuliko Kiswahili cha Kenya. Ni kweli kwamba wakenya wengi hata hawaongei vizuri Kiswahili cha Kenya. Lakini naamini kwamba wakenya wanaojishughulika na Wikipedia ya Kiswahili wanakijua. Ukifikiri kwamba mkenya ametumia Kiswahili kibaya hapa Wikipedia, taja mfano.
Lakini hakuna sababu yoyote ya kupendelea Kiswahili halisi ya Tanzania kuliko Kiswahili halisi cha Kenya. Kwa mfano, hakuna sababu ya kupendelea msemo "shule ya sekondari" kuliko msemo "shule ya upili".
Tushirikiane badala ya kutetana kwa asili ya utaifa. Marcos 00:54, 15 Oktoba 2006 (UTC)[jibu]

Uhusiano kati ya Kiingereza na Kiswahili

[hariri chanzo]
Nimeingiza maoni ya ndugu Thabit tena kwa vile ni sehemu ya majadiliano (nsingeiita "fujo"). Machoni mwangu yako sawa na mada ya Kiswahili cha Kenya hapo juu. Tuwaruhusu wengine kutoa maoni kuhusu matumizi ya lugha ya Kiswahili (ingawa kurasa nyingine za majadiliano zingefaa zaidi kuliko huu). --Oliver Stegen 11:18, 7 Machi 2007 (UTC)[jibu]

nchini Tanzania shule nyingi sana zinaanzishwa zinaitwa kwa kiingereza 'english medium schools' kikubwa kinachofundishwa ni watoto wanaosoma hapo kujua kiingereza. sasa juhudi za taifa kukikuza kiswahili zitafanikiwa ikiwa watoto wetu au kizazi kijacho kitakuwa kimeegemea sana katika kujua kiingereza? matokeo yanaanza kuonekana sasa maneno mengi ya misamiati ya kiingereza yameingizwa katika kiswahili na lugha yetu imeonekana kama inategemea lugha nyingine katika matumizi. kingine ni kwanini watanzania wasomi wanaokijua kiswahili wasitafsiri vitabu vingi vya lugha za kigeni katika kiswahili ili visaidie katika kukuza lugha yetu? wakoloni walivyokuja walijitahidi sana kuzijua lugha zetu na wakafanikiwa mfano mzuri ni vitabu vinavyo tumika makanisani katika vijiji vya mikoa mbalimbali vingi wakoloni ndio walivyoviandika baada ya kijifunza lugha yetu kwa nini sisi tunaoijua vyema lugha yetu tusitafsiri vitabu kama vya Sayansi,teknolojia na vitabu vya elimu mbalimbali katika lugha yetu ili viweze kueleweka na wasomaji wengi na visaidie kukikuza kiswahili? ninaomba wadau wa maswala haya wajitahidi kutendea kazi

Thabit Mikidadi, Dar es salaam