Majadiliano ya Wikipedia:Jamii

  Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
  Natafuta makala ya "Communist Manifesto" kwenye lugha ya Kiswahili.
  

  Makala 2000[hariri chanzo]

  Jamani tupeane hongera kwa kufikia makala 2000. Safari hii pongezi itakuwa hasa kwa Oliver aliyechapa kazi kwelikweli. Idadi kubwa katika wiki hizi mbili tu ni mkasi wa ajabu kabisa!!

  Haitakuwa rahisi kuendelea hivyo kwa sababu makala mengi yalikuwa makala za miaka na tarehe zilizoandaliwa kama fomu tu. Inabaki kazi nyingi kuzijaza kazi hii haitasukuma takwimu. Hata hivyo nimefurahi sana! --Kipala 16:19, 14 Septemba 2006 (UTC)Reply[jibu]

  sahihisho kuunganisha[hariri chanzo]

  inatoka Majadiliano_ya_Wikipedia:T173070Jamii: "How to download apps" --Simeone Deo 04:43, 3 Januari 2018 (UTC)Reply[jibu]

  Umuhimu wa kuutumia muda[hariri chanzo]

  Kwanini tunahitaji kuuthamini Muda? Mengi yamesemwa na bado mengine yanaendelea kuzungumzwa juu ya kitu kinachoitwa Muda. Najua sio jambo geni wala si mara yako ya kwanza kusikia pia , ninachotaka tujifunze pamoja hapa ni kuona kwa jinsi gani muda ni wa msingi kuweza ku control ratiba ya mtu katika kufanya kitu au jambo lolote lile akiwa na madhumuni ya kulikamilisha, elewa wazi sekunde moja ambayo unaweza ukaithamini inaweza ikaleta matokeo mazuri hasa pale utakapo gundua thamani yake. Ndio maana baadhi ya watu fulani hata siwezi kuwataja wamekuwa ni watu wa kuheshimu sana muda jambo linalopelekea wao kufanikiwa na kuwa watu wa juu siku zote, Kuna msemo moja mahali fulani una zungumza kuwa aliye mwaminifu katika vidogo huwa pia mwaminifu katika vilivyo vikubwa lakini vile vile asiye mwaminifu katika vilivyo vidogo katu hawezi kuwa mwaminifu katika vilivyo vikubwa.Jitafakari badilika alafu chukua hatua,usiwe mwepesi wa kuupoteza muda wala kuchezea ukitaka kufanikiwa. Richard Mboya (majadiliano) 09:57, 6 Septemba 2020 (UTC)Reply[jibu]