Majadiliano:Ukame
Mandhari
Habari ndugu, asante kwa kuendelea!! Naona numeanzisha makala kuhusu ukame. Basi kuna chanzo ingawa si makala nzuri bado makosa na kasoro, haiwezi kubaki jinsi ilivyo. Sasa naomba tushirikiane ili tufanye ukame kuwa makala inayofaa. Naomba twende pamoja. Fanya hatua zifuatazo:
- fanya neno la kwanza ("Ukame") kuonekana koze
- panga makala katika jamii. kuna jamii mbili ambazo ni Jamii:Metorolojia na pia Jamii:Maafa asilia
- unganisha makala na lugha nyingine. Hapo nenda chini kushoto kwa "Lugha" na chini yake kwa "Add links". Bofya hapo, utaona "Please select a site and a page that you want to link to this page. Language: ..."
- Katika nafasi ya "language" ingiza enwiki na chini yake kwa "page" ongeza drought. Utaona orodha ya maneno uthebitishe kwa click kwenye neno hilihili "drought". Sasa click "link with page" na uthebitishe tena.
- Baada ya kumaliza utaona orodha ya lugha upande wa kushoto wa dirisha (kama huoni bofya kwenye mshale mviringo juu katika dirisha la anwani, itafanya upya)
- Sasa nenda na tafuta kwenye lugha hadi unafika "simple English". (kama una matata kopi mstari unaofuata katika dirisha mpya / la pili)
simple.wikipedia.org/wiki/Drought
- fungua makala ya Drought katika Simple English , soma na utaona kasoro za jaribio lako. Tafsiri unavyoweza au uongeze kwa maneno yako mwenyewe.
- Halafu unijibu kwenye ukurawa wangu wa majadiliano kama unakwama au kufaulu, umwonyeshe pia Nd. Riccardo ukimwona. Kipala (majadiliano) 15:34, 16 Juni 2017 (UTC)