Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Ugali

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Samahani sijaelewa sentensi hii: Tonge la ugali hufinyangwa kwa mkono wa kushoto kisha kuchovya kwenye maziwa au mchuzi wa maharage. Kwa mazingira ya kawaida ususani Afrika ya Mashariki, Ugali huliwa kwa mkono wa kulia na sio wa "kushoto". Ila sijui kwa watu wa huko Ulaya chakula wao wanakichukuliaje, lakini kikawaida Ugali mkono wa kulia ni wa kulia na sio kushoto (mara nyingi huwa hovyo) ila sijui namna gani!--Mwanaharakati (majadiliano) 15:16, 16 Aprili 2008 (UTC)[jibu]

Twataka ushahidi juu ya Kusema kwamba ugali ni neno la Kirundi. Tangu kuzaliwa kwangu na kufuatilia kwangu masuala ya lugha hii, sijwahi kusikia kwamba Ugali ni neno la Kirundi. Tupewe ushahidi. Vinginenvyo, tutaondoa kipengele kile.--Muddyb MwanaharakatiLonga 12:07, 7 Desemba 2009 (UTC)[jibu]