Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Shubiri (kipimo)

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fasiri ya TUKI

[hariri chanzo]

TUKI inasema kwamba shubiri ni umbali kati ya kidole gumba na kidole cha kati. Nani ana hakika? ChriKo (majadiliano) 20:00, 18 Desemba 2014 (UTC)[jibu]

Sina uhakika lakini tafsiri ya Biblia katika Kiswahili inatumia "shubiri" katika sura ya 40 ya nabii Ezekieli, na neno la Kiebrania linamaanisha upana wa vidole vinne. Hata hivyo, Kamusi ya methali za Kiswahili inaeleza kwamba shubiri ni nafasi kati ya kidole kimoja na kingine (ila kidole cha gumba), na urefu wa umbali kati ya kidole cha gumba na kidole kingine huitwa "pima". Kwa vyovyote, inaonekana kama pima ni ndefu kuliko shubiri, yaani haiwezekani shubiri iwe umbali kati ya kidole cha gumba na kidole cha mwisho. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 05:34, 19 Desemba 2014 (UTC)[jibu]