Nenda kwa yaliyomo

Majadiliano:Mfumo wa Jua

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Majadiliano:Mfumo wa jua)

Atlasi yangu ya shule, pamoja na tovuti hii vinataja Utaridi = Pluto ("sayari" ya tisa). Matt Crypto 22:56, 12 Februari 2006 (UTC)[jibu]

Kumbe!! Nimeangalia [1]. Utaridi namna gani Pluto?? Pluto imejulikana tangu 1930 - pia kamusi Kiing-Kisw ya TUKI inatumia "Pluto". Lakini sishangai sana. Vitabu vya shule vya TZ... Ningeweka pesa kiasi kwa etimolojia yangu. Naona ingekuwa vema kumpata mtu katika TUKI huko DSM. Nimepata Utaridi katika kijitabu cha "Maajabu ya Ulimwengu" (kimetungwa na P. Sebald OSB, Benedictine Publications Ndanda-Peramiho 1985). Hata yeye anabadilishabadilisha Utaridi na Zebaki akitaja sayari ya kwanza. Lakini Pluto ni Pluto, hakuna njia kutumia jina la Kiarabu wakati Waarabu wenyewe hawana jina na kutumia lile la Kigiriki kipya, tena Utaridi inajulikana kabisa kuwa sayari ya kwanza??

Hata nisingeshangaa kama mtu amechanganya kila kitu ikawa utaratibu sasa. Kwa upande mwingine hadi sasa si watu wengi sana wanaotaja sayari kwa majina ya Kiswahili. Kwa hiyo itakuwa ajabu kwa wanahistoria ya lugha lakini haigusu watu wengi bado. Hata kuna uwezekano ya kwamba mkono mmoja (TUKI kamusi kiing-kisw) unasema kitu kimoja, halafu mkono mwingine (k.km. BAKITA au wizara ya elimu) unasema tofauti ilhali hawajui. Naona tuweke tuangalie watu wanasemaje tukusanye maoni kidogo. --Kipala 02:07, 13 Februari 2006 (UTC)[jibu]

Marekebisho kidogo: sayari ya Zuhura si Zebaki. Zebaki ni madini yanayoitwa Mercury katika lugha ya kiingereza, ambayo ni sayari ya Zebaki