Majadiliano:Kiesperanto
Mandhari
Wapendwa wala "lugha iliyopangwa" wala "lugha iliyotengenezwa" kwangu inaonekana kuwa Kiswahili sanifu. Kwa kweli Kiswahili ndiyo lugha mpya inona mabadiliko mengi.
Kwa ujumla mimi naona tufuate ushauri wa TUKI isipokuwa tukiweza kutaja sababu muhimu ya kudokeza TUKI walikosea au kuna njia nyingine yenye maana. Kwa lugha kama Esperanto TUKI imeshauri "Lugha bandia".
Je, kuna mtu anayepinga pendekezo hili; akipinga ni kwa sababu gani?? --Kipala 00:58, 1 Machi 2006 (UTC)
- Mimi ninapinga pendekezo hili. Neno "bandia" lina maana mbaya (kwa Kiingereza "imitation", "sham" "false"). Kusema kwamba Kiesperanto ni "lugha bandia" itaonekana kama kusema "Kiesperanto kinajaribu kuwa lugha, lakini kwa keli siyo lugha".
- Katika lugha nyingine pia kuna msukano kuhusu maneno sahihi kwa lugha kama Kiesperanto. Kwa mfano, kwa Kiingereza wengine wanatumis "artificial language", lakini kwa kawaida Waesperanto wanapinga utumizi huu, kwa sababu "artificial" pia ina maana mbaya kidogo. Kwa hiyo Waesperanto wanapenda kutumia "planned language".
- Siku hizi, msemo "planned language" linatumika kwa lugha zile ambazo zilitengenezwa kwa ajili ya utumiaji wa kawaida baina ya watu, na "constructed language" linatumika kwa lugha zote zilizotengenezwa. Mimi ninaamini kwamba ni nzuri kuwa na msemo kama "planned language" kwa Kiswahili. Niliamua kutumia "lugha iliyopangwa", lakini pia inawezekana kusema "lugha mpango" au "lugha ya mpango". Mimi sina uhakika ipi ni nzuri zaidi. Marcos 01:04, 3 Machi 2006 (UTC)
- Nimewahi kuandika huko "Talk:Lugha iliyotengenezwa" juu ya swali hili. Ninakubali ya kwamba "Lugha bandia" si chaguo zuri la TUKI. Inaonekana mtu alijaribu kutafsiri neno bila kuangalia upana wa maana yake pande zote mbili. Lakini hatuna budi kujitahadhari tusiunde maneno mapyamapya bila kujali utaratibu na muundo wa lugha. Sisi wachangia wikipedia ni watu wachache mno tena wengi wasio Waswahili au tukiwa Waswahili tuko mbali na mazingira penye Kiswahili hai.
- Ushauri wangu ni hivi: a) tufuate mapendekezo ya TUKI kama yapo; b) tukiona sababu ya kutokubali tuandike makala lakini tutoe maelezo kwenye ukurasa wa majadiliano c) tuone majadiliano tuombe hasa waswahili wazawa washauri
- Kuhusu lugha ningeshauri "lugha ya kuundwa" au "lugha ya kupangwa".
- Zaidi ya hayo sielewi unataka kudokeza nini kwa kutuletea makala juu ya "lugha iliyotengenezwa" pamoja na "lugha iliyopangwa". Tofauti yake haieleweki kufuatana na majina haya. Kuhusu maneno yenyewe ni sawa kabisa kuyatumia ndani ya sentensi lakini ningeona hayafai vema kuwa majina. Pia makala ya "lugha saada" - nafikiri unamaanisha kitu kama "lugha saidizi"? Ningefurahi kama wengine wangechangia! --Kipala 19:18, 5 Machi 2006 (UTC)
- Ninakubali na ushauri wako kuhusu kuwafuata TUKI tusipokuwa na sababu maalum ya kutowafuata.
- Pia ninakubali na matumizi ya "lugha ya kuundwa", "lugha ya kupangwa" na "lugha saidizi".
- Misemo "lugha ya kuundwa" na "lugha ya kupangwa" haionyeshi vizuri tofauti ya maana kati ya misemo hii, lakini licha ya hiyo tuitumie. Lugha nyingi zinatumia misemo inayofanana (en: constructed language and planned language; de: konstruierte Sprache und Plansprache; eo: konstruita lingvo kaj planlingvo), na tofauti kati ya hizi ni muhimu. Lazima tuwe na tofauti kama hii kwa Kiswahili, na mimi siwezi kuona njia nzuri zaidi kuliko kutumia "lugha ya kuundwa" na "lugha ya kupangwa". Marcos 17:27, 8 Machi 2006 (UTC)
- Sasa nimefanya mabadilisho haya:
- "lugha iliyotengenezwa" --> "lugha ya kuundwa"
- "lugha iliyopangwa" --> "lugha ya kupangwa"
- "lugha saada ya kimataifa" --> "lugha saidizi ya kimataifa"
- Sasa nimefanya mabadilisho haya: