Majadiliano:Karagwe

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Naomba kutoa ufafanuzi kidogo. Karagwe sio utemi mdogo wa kabila la Wahaya kama ilivyoelezwa hapo juu. Karagwe Kwa asili ni wilaya ya kabila la Wanyambo(Ab'hanyambo) na lugha yao ni Orunyambo. Kuwaita Wahaya ni kuwanyang'anya haki yao ya msingi ya kuwa kabila kubwa na huru linalojitegemea. Kuna Wahaya wachache waliohamia Karagwe katika harakati za kutafuta makazi na udongo wenye rutuba, nao wamejikita sana maeneo ya Keiso(Kaisho) na Mab'hira(Mabira) Upo ushaidi wa kutosha wa maandishi unaoelezea kabila la Wanyambo na jinsi mwingiliano wao na makabila mengine ulivyokuwa. Kwa maelezo zaidi soma kitabu cha Profesa Israel Katoke "The Karagwe kingdom" na Tanganyika Notes and Recods ya 1947" ukurasa wa 8-26.

Iliongezwa na mtumiaji asiyejiandikisha 196.41.59.62 tarehe 19 Juni 2009 (hariri) (tengua)