Majadiliano:Habari za uumbaji
Mandhari
"kidhehebu" nini? Hiyo Kiswahili? (imeandikwa na user:CarlHinton 12:06, 4 Julai 2008)
- Ndiyo. Maana yake: makala inatumia hoja la kikundi fulani cha kidini - kutoka "madhehebu/ dhehebu" (Kar. مذهب madhhab). Ukipenda kujadili matumizi haya heri uendelee kwenye ukurasa wa Template_talk:Kidhehebu.
- Kuhusu matumizi ya templeti hii hapo tatizo ni wazi: Umenakili maandishi moja kwa moja kutoka kwa tovuti hii; yaliyomo ya tovuti inaonekana sawa na kitabu cha "Biblia Inasema - Ufafanuzi wa Neno la Mungu kwa watu wa siku hizi" kilichoandikwa na Don Fleming. Hiki ni kitabu kinacholenga kuonyesha jinsi gani Mkristo anaweza kuelewa Biblia kufuatana na wazo la mwandishi huyu. Ni mwaliko kwa imani ya Kikristo, kinatangaza imani.
- Kwa hiyo kamusi elezo kama wikipedia si mahali pake. Ukipenda kujua zaidi soma Msaada wa kuanzisha makala au ukipendelea kusoma Kiingereza en:Wikipedia:What_Wikipedia_is_not. Hatujaanzisha bado wikimaktaba (wikisource) kwa Kiswahili ambako ni mahali pa vitabu. Masharti ya makala ni: ieleweke kwa kila mtu na hatujali msomaji ana imani au dini au utamaduni gani.
- Kwa hiyo makala hii pamoja na sehemu ya makala ulizoweka haitakaa kwenye wikipedia hii isipobadilishwa sana.
- Menginevyo naomba uweke sahihi pale unapoandika. Bonyeza tufe la kumi au alama zifuatazo --~~~~ zitaonyesha jina lako na tarehe baada ya kuhifadhi andishi. --Kipala (majadiliano) 13:18, 5 Julai 2008 (UTC)