Majadiliano:Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mabadiliko - tuwe waangilifu[hariri chanzo]

Naomba tuwe waangilifu wakati wa kufanya masahihisho. Katika orodha ya nchi mabadiliko kadhaa yametokea yasiyofaa. Kwa mfano kurejea jina la Ethiopia kwa "Uhebeshi". Uhebeshi si Kiswahili. Kuna neno "Uhabeshi" - sawa tukijadiliana neno lipi linafaa zaidi kati ya Uhabeshi au Ethiopia.

Au: Kurejea Msumbiji kwa "Mozambik". Mozambik si Kiswahili hata kidogo, na makala ya Msumbiji ilikuwepo tayari. Sasa kiungo hiki kimevunjwa.

Naomba kabla ya kubadilisha neno tuone kwanza kama kiungo kipo tayari (rangi ya neno kuwa buluu). Kama kipo hatuna budi kubadilisha kiungo pia. Menginevyo tunajenga matata katika kamusi yetu! Lakini tukitaka kubadilisha ni vema kuhakisha kwa kamusi kama mwezetu labda alikuwa na sababu nzuri za kuandika jinsi alivyoandika. Kam kuna wasiwasi basi tuandike kwanza katiuka ukurasa wa majadiliano tutaje sababu zetu halafu tusubiri. --Kipala 18:55, 19 Aprili 2006 (UTC)

Tukubaliane kwanza majina ya nchi. Kwa maoni yangu majina yanayofuata ni sahihi:
 • Mauritius - Morisi
 • Réunion - Riyunioni
 • Sudan - Sudani
 • Cameroon - Kameruni
 • Guinea - Gine
 • Gabon - Gaboni
 • Algeria - Aljeria
 • Lesotho - Lesoto
 • Benin - Benini
 • Cape Verde - Kepuvede
 • Ivory Coast - Kotivaa
 • Mauritania - Moritania
 • Niger - Nijeri
 • Nigeria - Nijeria
 • Senegal - Senegali
 • Sierra Leone - Siera Leoni ChriKo 22:32, 7 Oktoba 2006 (UTC)

Tusipoteze nguvu zetu kuvutana juu ya majina ya kijiografia[hariri chanzo]

ChriKo, asante kwa ushauri wako. Ushauri wangu ni tofauti kidogo: tusivutane mno kuhusu tahijia ya maneno au kutumia majina namna gani. Tutapoteza muda wetu tu.Tuongeze maumbo mengine kwa kuongeza makala za "Redirect".
Sababu zangu
 • hali halisi hakuna orodha ya majina inayokubaliwa. Hatuna budi kuendelea na maumbo mbalimbali lakini tuweke viungo! Tujitahadhari tukibadilisha kitu ili tusiharibu viungo vilivyopo!
 • orodha za TUKI na BAKITA ya majina ya nchi haifuatwi mara nyingi wala Tanzania wala Kenya. Jinsi inavyoonekana kwangu sehemu yake ni kazi bure. Kama orodha ya Kamusi Hai ni sawa zote mbili hazikubaliani kati yao.
 • Nimejipatia "Atlasi kwa Shule za Msingi Tanzania" (ISBN 9976950403, chapa ya tatu 2005) ambayo ni Atlasi ya pekee kwa Kiswahili ninayofahamu. Haifuati orodha ya TUKI. Lakini hii ni namna ya majina ambayo wanafunzi wanafundishwa nchini Tanzania.
 • inaonekana kuna nchi yenye majina ya pekee kwa Kiswahili yenye uzoefu ya miaka mingi (kwa mfano Misri, Uingereza, Marekani, Shelisheli). Haya tutetee.
  • Nchi nyingine ina majina ya kimapokeo (kama vile Uhabeshi, Uajemi) lakini kuna matumizi sawasawa ya majina ya kimataifa kama vile Ethiopia na Iran. Hatuna budi kuonyesha yote.
  • Kuna nchi nyingine ambazo hazijadiliwi mara nyingi kwa Kiswahili. Hapo matatizo yanaonekana ya orodha zilizotungwa kwenye deski ya TUKI au BAKITA lakini hazitumiki au hutumiwa mara chache sana lakini majina ya kimataifa hutumiwa zaidi. Mifano ni Guinea, Cote d'Ivoire, Nigeria (TUKI: Gini, Kodivaa, Nijeria) na mengi mengine. Nashauri tuongeze Redirect na kuongeza kwa mabano majina haya katika makala ya nchi.
 • Mtindo wa TUKI na BAKITA mara nyingi ni kufuata matamshi ya Kiingereza. Ila tu si rahisi kuelewana kwa sababu katika Kiingereza kuna tofauti katika matamshi (Kiingereza ya kisiwani au ya Marekani auya wapi..). Wameanza tu kwa orodha ya majina machache ya nchi. Baada ya kuandika makala mengi ya nchi naona matata katika mtindo huo. Pamoja na sababu nilizotaja hapo juu inaongeza ugumu wa kuoandika makala upande wa historia, kwa mfano ukieleza asili ya jina la nchi (etimolojia). Kwa mfano Guyana ilipatikana kama jina la koloni tatu za Uingereza, Ufaransa na Uholanzi katika Amerika ya Kusini. Kwa nini tuandike nchi moja "Guyana" lakini nchi nyingine "Gwiyana" (TUKI)?? Kwa nini San Marino iwe "Samarino"?? Hizi ni fikra tupu za deski lakini si matumizi ya lugha.
Nitaandika makala kuhusu tatizo na kutoa orodha ya majina ya nchi kandokando. Nimeshandaa orodha ya TUKI/BAKITA kwa bara na nitaongeza umbo la Atlasi kwa Shule za Msingi.
Naona heri tufuate umbo la Atlasi kwa sababu hii ni kitabu kinachotumiwa, tofauti na orodha zile zilizotajwa. Unaonaje ? --Kipala 18:31, 8 Oktoba 2006 (UTC)
Kipala, nimefahamu sababu zako za kupea nchi majina fulani. Lakini nafikiri si mzuri kutumia kitabu kimoja ili kuchagua majina haya. Ni kweli kama wanaisimu hawakubali kuhusu utumiaji wa majina ya nchi. Hata mimi sipendi majina kadhaa, kama Gine na Kotivaa (hata Samarino). Wala sipendi mtindo wa kufuata matamshi ya Kiingereza. Lakini nani atachagua? Ni sisi wazungu au wazungumzaji wa kienyeji? Inaonekana kwangu kama ni lazima tuhakikishe utumiaji wa majina ya nchi miongoni mwa wananchi na kwa magazeti.
Tusipotumia majina ambayo yanafuata matamshi ya Kiingereza, tutafuata matamshi gani? Kama hakuna jina ambalo linatumika sana, labda tungetumia jina rasmi linalotumika nchini, k.m. Guyana au San Marino. Pengine tunaweza kufuata majina yanayotumika kwa lugha zingine za Bantu. K.m., “Kameruni” hutumika kwa Kinyarwanda. Nafikiri afadhali tutie –i nyuma ya majina rasmi ambayo mwisho yao ni konsonanti, kwa sababu hii haipatikani kwa maneno ya lugha za Bantu.
Kwa kila hali haya ni majadiliano baina ya wazungu wawili. Afadhali tukaribishe wananchi. ChriKo 21:38, 9 Oktoba 2006 (UTC)