Vimatu, matumatu au maige ni wana au tunutu wa panzi. Wanafanana na panzi wapevu lakini ni wadogo zaidi na mabawa yao hayajakomaa.