Mai bint Mohammed Al Khalifa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Shaikha Mai Bint Mohammed Al Khlida

Mai bint Mohammed Al Khalifa aliteuliwa kama waziri wa mawasiliano nchini Bahrain mwaka 2009.

Alikuwa mwanamke wa kwanza kuwa waziri wa mawasiliano nchini Bahrain. Yeye ni mweyekiti wa bodi ya 'Arab Regional Center for World Heritage' na pia ni rais wa mamlaka ya tamaduni na maliasili ya Bahrain. Mwaka 2014 jarida la Forbes la mashariki ya kati lilimtaja kama kati ya wanawake wenye ushawishi wenye asili ya kiarabu.Kama waziri wa tamaduni alijitahidi kufanya kazi na wasanii wa Bahrain. Kwenye siku ya kumbukumbu ya makumbusho ya kidunia tarehe 21 Oktoba 2015 jijini New York, Mai bint Mohammed Al Khalifa alipewa tuzo kutokana na jitihada za kuhifadhi maeneo ya makumbusho na tamaduni za Bahrain. Mwaka 2017 aliteuliwa kama balozi wa kimataifa wa mwaka katika maswala ya utalii wa maendeleo na Umoja wa mataifa.

Mwaka 2020, Sheika Mai aliteuliwa na serikali ya Bahrain kama katibu mkuu wa taasisi ya utalii wa kidunia.Januari 2021, aliekuwa anashikilia wadhifa wa katibu mkuu Zurab Pololikashvili alishinda uchaguzi.

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mai bint Mohammed Al Khalifa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.