Nenda kwa yaliyomo

Maendeleo Vijijini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kilimo ni mojawapo ya shughuli ya maendeleo vijijini

Maendeleo ya vijiji ni mchakato wa kuboresha hali ya maisha na ustawi wa kiuchumi wa watu wanaoishi vijijini, mara nyingi maeneo yaliyotengwa na yenye watu wachache.[1] Mara nyingi, vijijini kuna umaskini mkubwa kuliko mijini kutokana na uhaba wa shughuli za kiuchumi, na ukosefu wa uwekezaji katika miundombinu muhimu kama vile elimu.

Maendeleo ya vijijini yamejikita katika matumizi ya maliasili zinazohitaji ardhi kama vile kilimo na misitu. Hata hivyo, mabadiliko katika mitandao ya uzalishaji ulimwenguni na ukuaji wa miji kumepelekea kubadilisha vijiji. Utalii wa vijiji, biashara ndogondogo, na burudani vimechukua nafasi ya uvunaji wa rasilimali na kilimo kama vichocheo vikuu vya uchumi.[2] Jamii za vijijini zinatakiwa kuangalia maendeleo kwa mtazamo mpana zaidi, na kuongeza umakini kwenye malengo mbalimbali ya maendeleo badala ya kutoa motisha tu kwa biashara za kilimo au zinazohusiana na maliasili. Elimu, ujasiriamali, na miundombinu huchukua nafasi muhimu katika kuendeleza maeneo ya vijijini.[3] Sifa nyingine ya maendeleo ya vijiji ni msisitizo wake katika uzalishaji wa bidhaa wa ndani.[4] Tofauti na maeneo ya mijini, ambayo yanafanana kwa mambo mengi, maeneo ya vijijini hutofautiana sana.Kwa sababu hii, kuna mikakati mbalimbali ya maendeleo ya vijijini inayotumika duniani kote.


Vikundi vya maendeleo vijijini

[hariri | hariri chanzo]
  1. Moseley, Malcolm J. (2003). Rural development : principles and practice (1. publ. ed.). SAGE. p. 5. ISBN 9780761947660.
  2. Ward, Neil; Brown, David L. (1 December 2009). "Placing the Rural in Regional Development". Regional Studies. 43 (10): 1237–1244. Bibcode:2009RegSt..43.1237W. doi:10.1080/00343400903234696.
  3. Rowley, Thomas D., ed. (1996). Rural development research : a foundation for policy (1. publ. ed.). Greenwood Press. ISBN 9780313297267.
  4. Moseley, Malcolm J. (2003). Rural development : principles and practice (1. publ. ed.). SAGE. p. 7. ISBN 9780761947660.