Maduka ya Gee Bee
Maduka ya Gee Bee | |
---|---|
Jina la kampuni | Maduka ya Gee Bee |
Ilianzishwa | 1906 |
Mwanzilishi | Ndugu wa Familia ya Glosser |
Huduma zinazowasilishwa | Uuzaji wa bidhaa mbalimbali |
Makao Makuu ya kampuni | Johnstown, Pennsylvania |
Nchi | Marekani |
Kampuni ya maduka ya Gee Bee ilianza Johnstown, Pennsylvania, Marekani,katika mwaka wa 1906. Ilianzishwa na ndugu wa familia ya Glosser walipofungua duka la chumba kimoja katika jengo la Franklin Building. Kampuni iliunda matawi yake katika miaka ya 1950 wakifungua maduka ya Gee Bee. Mengi ya maduka haya,pia lile la kwanza, yaliyokuwa na jina la Glosser yalibaki wazi katika miaka ya 1980. Jengo la Franklin Building liliendelezwa katika miaka ya katikati ya 1990. Maeneo ya maduka ya Gee Bee yaliuziwa minyororo mingine ya maduka katika miaka ilyofuata. Eneo la Eastland Mall katika Versailles Kaskazini,Pennyslvania,liliacha kutuika kabisa na likatumika kama soko hadi 2005. Eneo la Washington,Pennsylvania lilibadilishwa usimamizi mara kadhaa(hivi sasa ni duka la Gabriel Brothers) lakini bado lina muundo uo huo wa Gee Bee.
Eneo la tatu lililokuwa University Park Centre, mjini Richland,Johnstown,Pennyslvania. Duka lilifanyiwa ukarabati mkubwa katika miaka ya 1990, muda mfupi kabla ya kufungwa kisha kufunguliwa kama Duka Kubwa la Giant Eagle,ambalo limebaki hivyo hadi sasa. Nje ya duka hilo bado linafanana na lile la Gee Bee,lakini ndani ya duka limebadilishwa kabisa. Eneo jingine mjiniGreensburg,Pennyslvania,pia , lilibadilishwa kuwa Duka jingine Kubwa la Giant Eagle baada ya Gee Bee la hapo kufungwa.
Aidha, duka la nguo za watoto la Gee Bee lililokuwa Westwood Plaza katika eneo la Upper Yorder,kitongoji kilicho nje ya Johnstown. Duka hilo lilifunga biashara lake katika mwaka wa 1993 na likabomolewa. Hivi sasa, Monro Muffler ipo katika nafasi hiyo pahali duka hilo lilikuwa hapo awali.
Katika kata la Richland, toleo la manjano kubwa lilikuwa karibu na barabara ya Eisenhower Boulevard. Nembo ya kampuni hii ilikuwa katuni msichana mwenye amevaa kofia ya safari akiwa ametabasamu.
Duka la Gee Bee lililokuwa katika eneo la Fairlane Village Mall katika Pottsville,Pennyslvania na moja katika Church Hill Mall katika Hazleton,Pennyslvania, yalikuwa maduka ya Value City. Ilipofika mwisho wa miaka ya 2008,yote mawili yamefungwa,pamoja na maduka mengine yote ya Value City.
Duka jingine, katika Center Township, Pennyslvania lilifungwa katika miaka ya 1980.
Duka la Gee Bee lililokuwa Altoona na likawa duka msingi ya Park Hills Plaza. Duka hilo lilifungwa katika mwanzo wa miaka ya 1990, pahali hapo palikuwa wazi kwa muda fulani. Jengo hilo liligawanywa na sasa linatumika na Duka la Dunham's Sporting Goods na duka la Toys 'R Us.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Gee Bee ya mtaa haijaathiriwa na kufungwa kwa maduka mengine Ilihifadhiwa 25 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.
- Ukarabati kwa jengo la Glosser Brothers Ilihifadhiwa 9 Julai 2006 kwenye Wayback Machine.
- 1990 Glosser Brothers Ilihifadhiwa 15 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.