Madeleine Bates

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Madeleine Ashcraft Bates (amezaliwa 1948) ni mtafiti wa uchakataji wa lugha asilia ambaye alifanya kazi katika kampuni ya BBN Technologies huko Cambridge, Massachusetts kuanzia mwanzoni mwa miaka ya 1970 hadi mwishoni mwa miaka ya 1990. Yeye alikua raisi wa chama cha waandishi wa lugha ya kompyuta mwaka 1985, na mhariri mwenza wa kitabu Challenges in Natural Language Processing (1993).

Elimu na taaluma[hariri | hariri chanzo]

Bates alikuwa mwanafunzi katika Chuo cha Allegheny kabla ya kuhamishwa kwenda Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon, ambapo alijifunza hisabati, na kuhitimu mwaka 1968. Alikamilisha Ph.D. yake ya hisabati katika Chuo Kikuu cha Harvard mnamo mwaka 1975, akifanya kazi huko pamoja na Bill Woods juu ya mabadiliko ya mitandao kuongezeka.

Akiwa mwanafunzi huko Harvard, yeye alianza kufanya kazi za muda mfupi katika kampuni ya BBN mnamo mwaka 1971. Baada ya kumaliza Ph.D., alikuwa profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha Boston kwa miaka mitatu kabla ya kuwa mtafiti kamili katika kampuni ya BBN.

Maisha yake binafsi[hariri | hariri chanzo]

Bates aliolewa na mkemia Alan Hunt Bates katika majira ya joto mnamo mwaka 1968; baadaye akawa profesa katika Chuo Kikuu cha Massachusetts Dartmouth . Mama yake, Madeleine DeMuth Ashcraft (aliyefariki 1990), alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa unaoitwa Huntington's disease kwa muda mrefu na Bates amekuwa mwanaharakati wa matibabu ya ugonjwa huo, akifanya kazi kama raisi wa Massachusetts Chapter ya Tume ya Kupambana na Ugonjwa unaojulikana kama Huntington's disease.

Machapisho yaliyochaguliwa[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]