Nenda kwa yaliyomo

Mabantu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mabantu
Twaah (aliyesimama) na Muuh Mabantu (aliyechutama) wakiwa katika seti ya Tamasha la Nandy—2021.
Taarifa za awali
Kazi yakeWanamuziki
Miaka ya kazi2018
Ameshirikiana naWhozu, Young Lunya, R the DJ

"Mabantu" ni jina linalolitambulisha kundi la muziki wa Bongo Flava kutoka jijini Dar es Salaam, Tanzania.[1] Kundi linaundwa na wasanii wawili, Twarha Kanengo (Twarha Mabantu 9 Julai, 1997) na Mwarami Kajonje (Muuh Mabantu-21 Januari, 1999).

Kwa pamoja, wanafahamika kwa wimbo wao Sundi (2018), Bodaboda (2018) "Kama Tulivyo" (2019) wakimshirikisha Whozu,Mali safi (2024)[2], na ule maarufu zaidi ni Nawakera walishirikiana na Young Lunya. Pia waliwahi kufanya kazi ya kishirikishi na R "the" DJ, Shobo (2021).

Mabantu walikuja kutambulika zaidi kupita wimbo wao wa Sponsa (2020), walirudi tena na Young Lunya.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Hapo awali, wawili hawa wote walikuwa katika taasisi ya Said Fella, maarufu kama "Mkubwa na Wanawe" wakiwa sehemu ya wasanii wanaosubiri kuwezeshwa. Ilipotimu mnamo mwaka wa 2013, kabla hata ya kushiriki katika wimbo hata mmoja, vijana hawa waliamua kuondoka mikononi mwa mkubwa na wanawe, na hatimaye kuanzisha Mabantu rasmi.

Mwarami aliingia Mkubwa na Wanawe mwishoni mwa 2011, wakati Twarha aliingia 2012 mwishoni. Lakini lilipokuja suala la kutaka kujiendeleza zaidi nje ya mikono ya kituo cha Mkubwa Fella, iliwalazimu waje na jina la kundi ambalo wangelitumia kama utambulisho kwa wasanii hawa.

Wakiwa kituoni kwa Fella, walipata fursa ya kushiriki mazoezi mbalimbali ya kuondoa uwoga wa hadhira na matumizi ya ala za sauti na vyombo vya muziki. Kituo kilikuwa na kila aina ya vifaa wezeshi kwa watoto wanaokaa hapo. Walirekodi nyimbo kadhaa ambazo hazikutoka nje ya kituo hicho. Kimsingi, Twarha ni mnenguaji na mwimbaji, wakati Mwarami alijipambanua kama mwimbaji zaidi.

Nyimbo maarufu

[hariri | hariri chanzo]

Hizi ni baadhi ya nyimbo za Mabantu.

Caption text
Na. Jina la wimbo Maelezo
1. Umenuna
2. Hachiti
3. Nawakera
4. No Love No Stress
5. Show Show
6. Sina Shida Nae
7. Happy Birthday
8. Mguu Pande
9. Mwendo
10. Amina
  1. "EXCLUSIVE: Tazama Mabantu wakichambua mistari ya wimbo wa 'Sundi' – Dar24" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-10-02.
  2. "Mabantu wafunguka kuhusu Whozu kukatwa nywele | East Africa Television". www.eatv.tv. 2019-03-26. Iliwekwa mnamo 2021-10-02.
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mabantu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.