Maasai Market

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Maasai Market

Maasai Market ni mojawapo ya soko zinazojulikana zaidi mjini Nairobi. Soko hili hushughulika na uuzaji wa michoro, nakshi, vito, maguo yenye asili ya kiafrika na kadhalika.

Maasai Market liko katika jiji la Nairobi kinyume cha njia ya kuzunguka kubwa zaidi barani Afrika cha 'Globe'. Soko hili hufunguliwa siku maalum za wiki, Jumanne na Jumamosi kuanzia saa kumi na muja asubuhi hadi saa mbili usiku. Pia huwa katika maduka makubwa yaliyo katika mazingira ya Nairobi, Village Market siku ya Ijumaa na Yaya Center siku ya Jumapili. Soko hili huwa na wauzaji wengi sana na kwa hivyo huwa kubwa sana

Historia[hariri | hariri chanzo]

Maasai Market ilianzia kama vutio la watalii ambapo watalii walienda kujionea wamaasai kama wamevaa vito na nguo zao za kitamaduni. Hili lilivutia watu wengi sana waliokuja kujionea na wengine waliokuja kununua vitu hivi.

Wauzaji katika soko hili ni wa kirafiki sana na wenye furaha tele. Hutakosa kuwaona wamaasai waliovalia nguo zao za kitamaduni na vito. Tamaduni hii hufurahiwa na watu wote bila kuzingatia asili. Nchini kenya, watu wengi huvalia nguo za kimaasai za kitamaduni hata kama wao si wamaasai. Jambo hili linaonyesha jinsi tamaduni hii inapendwa na wengi na hili huimarisha umaarufu wa soko hili.

Ukija Kenya, usisahau kutembelea soko hili ili ujiunge nasi katika kusherehekea tamaduni hii.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]