Gregor Mendel : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '250px|thumbnail|Gregor Mendel katika sare ya mmonaki '''Gregor Johann Mendel''' (Heinzendorf, Austria,<ref>sasa H...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 21:21, 14 Juni 2014

Gregor Mendel katika sare ya mmonaki

Gregor Johann Mendel (Heinzendorf, Austria,[1] 20 July 1822 – Brünn, Austro-Hungary,[2] 6 January 1884) alikuwa mmonaki na mtaalamu wa botania nchini Austria.[3]

Anakumbukwa kama mwanzilishaji wa elimu ya jenetikia kwa utafiti wake katika njegere. Alitambua mfumo wa urithi wa tabia thabiti na tabia dhaifu. Mfumo huu alieleza kwa mafundisho yanayojulikana leo kama sheria ya urithi ya Mendel.

Utafiti wake wa njegere

Mendel alitumia njegere zenye tabia mbalimbali: kwa mfano aina fupi na ndefu, zenye rangi njano au kibichi, zenye maua ya rangi tofauti.

Akizalisha aina hizi kwa kuzichanganya aliona ya kwamba kizazi cha pili cha mchanganyiko kilionyesha tabia moja tu maana tabia thabiti ilishinda na tabia dhaifu haikuonekana tena. Lakini alipoendelea kuzalisha njegere za kizazi cha pili matokeo katika kizazi cha tatu zilikuwa tofauti. Hapa tabia dhaifu ilitokea tena.

Mendel aliendelea kuzalisha njegele na kuandikwa takwimu jinsi gani tabia tofauti zilitokea katika vizazi vya pili na vya tatu. Aliona mwanzoni ya kwamba katika kizazi cha tatu 3/4 zilionyesha tabia thabiti na robo 1 tabia dhaifu. Lakini alipoendelea kuzalisha katika kizazi kifuatachom alijifunza kuwa ya kwamba robo mbili ziliendeleza tabia 1 tu (ama ndafu/fupi au au njano/kibichi n.k.) na nusu iliyobaki iliweza tena kuleta tabia zote mbili katika kizazi baadaye . Kwa hiyo katika kizazi hiki robo mbili zilikuwa safi kitabia na nusu ilikuwa na tabia chotara.

Hapo aligundua ya kwamba tabia zinaendelezwa kwa kipimo cha 1:2:1 yaani 1 safi A : 2 chotara AB : 1 safi B.

Hapo ilithebitika ya kwamba katika kuzalisha tabia tofauti hizi hazichanganya tu lakini bado zote mbili zilikuwepo na kutokea katika vizazi vya baadaye. [4][5][6]

Mendel aliandika kitabu juu ya utafiti wake mwaka 1866 lakini wakati ule watu hawakuelewa bado umuhimu wake. Jenetikia ya kisasa ilianza miaka 35 baadaye wakati kazi za Mendel zilisomewa tena.[7]

Marejeo

  1. sasa Hynčice, Czech Rep
  2. now Brno, Czech Rep
  3. "Gregor Mendel". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 2007-4-4.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. Stern, Curt and Sherwood, Eva R. (eds) 1966. The origin of genetics: a Mendel source book. Freeman, S.F.
  5. Carlson, Elof Axel 1966. The gene: a critical history. Saunders.
  6. Olby, Robert 1985. Origins of Mendelism, 2nd ed. Chicago.
  7. Henig, Robin Marantz 2000. A monk and two peas: the story of Gregor Mendel and the discovery of genetics. Weidenfeld & Nicolson, London.
  • Iltis, Hugo 1932. Life of Mendel, transl. by Eden & Cedar Paul. Allen & Unwin, London. German original: Gregor Mendel: Leben, Werk und Wirkung. Springer, Berlin 1924.

Viungo vya Nje