Perpetua Mtakatifu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d roboti Nyongeza: ro:Perpetua şi Felicitas
d roboti Badiliko: fr:Perpétue
Mstari 22: Mstari 22:
[[en:Perpetua and Felicity]]
[[en:Perpetua and Felicity]]
[[eo:Perpetua kaj Feliĉita]]
[[eo:Perpetua kaj Feliĉita]]
[[fr:Sainte Perpétue]]
[[fr:Perpétue]]
[[hu:Szent Perpetua]]
[[hu:Szent Perpetua]]
[[it:Sante Perpetua e Felicita]]
[[it:Sante Perpetua e Felicita]]

Pitio la 06:25, 3 Agosti 2008

Picha ya Perpetua (mnamo 1280 katika kanisa la Porec - Kroatia)

Perpetua (181 - 7 Machi 203) alikuwa kijana na mama mjini Karthago wakati wa Dola la Roma aliyeuawa kama mshahidi wa imani ya Kikristo. Aheshimiwa kati ya watakatifu wakristo na sikukuu yake ni 7 Machi.

Perpetua akumbukwa pamoja Felista na vijana watatu wanaume akiuawa pamoja nao.

Perpetua alikuwa binti wa familia tajiri. Kwa umri wa miaka 22 aliolewa na kuwa na mtoto mdgo. Wakati ule alijiandaa kubatizwa pamoja na watumishi wake Felista na Revocatus na kijana mwingine aliyeitwa Saturnius. Walikamatwa pamoja na mwalimu wao Saturus katika wimbi ya mateso ya Wakristo chini ya serikali ya Kaisari Septimius Severus (193-211).

Mwanzoni Perpetua alifungwa ndani na kupewa nafasi ya kuachana na imani yake. Alipokataa alihukumiwa kifo pamoja na wenzake. Gerezani walipokea ubatizo.

Historia ya Perpetua ni ya pekee kwa sababu kuna kumbukumbu zinazosimulia habari zake gerezani na wataalamu huamini ya kwamba zimeandikwa na Perpetua mwenyewe. Kama hii ni kweli ni maandiko ya kale kabisa ya mwanamke Mkristo katika historia iliyotunzwa.

Perpetua alibembebelezwa sana ba babaye aachane na Ukristo na kuokoa maisha yake lakini alikataa.

Pamoja na wenzake aliuawa katika uwanja wa michezo mbele ya watu wote. Hukumu ilitekelezwa kwa wanyama witu wa pori.