Uhamiaji wa binadamu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Created by translating the page "Human migration"
(Hakuna tofauti)

Pitio la 19:56, 4 Agosti 2018

Kiwango cha uhamiaji

Uhamiaji wa binadamu ni watu kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa nia ya kuanzisha makazi ya kudumu au ya muda katika eneo jipya. Kwa kawaida, watu husafiri masafa marefu, ndani mwa nchi au kutoka nchi moja hadi nyingine. Watu wanaweza kuhama kama watu binafsi, kama familia au katika makundi makubwa.[1] Mtu anayetoroka maafa ya asilia au vita vya wenyewe kwa wenyewe huitwa mkimbizi au mkimbizi wa ndani kwa ndani kama anahamia ndani mwa nchi. Pia, kuna watu ambao hutafuta kimbilio kutokana na kuteswa kwa ajili ya msimamo wa kisiasa au dini.

Wahamahamaji hawachukuliwi kuwa wahamiaji kwa kuwa hawana nia ya kufanya makazi na kuhama kwao ni kwa msimu tu.  Pia, shughuli za watu kusafiri kwa madhumuni ya utalii, usafiri au hija sio uhamiaji.

Takwimu za uhamiaji

Sehemu ya wahamiaji katika kila nchi ya ulimwengu katika mwaka 2015.[2]

Makadrio kadhaa ya takwimu za uhamiaji katika dunia yapo.

Benki ya Dunia huchapisha takwimu zake katika Migration and Remittances Factbook kila mwaka tangu mwaka 2008.[3] Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) huchapisha Ripoti ya Dunia Uhamiaji kila mwaka tangu mwaka 1999. Idara ya Takwimu Ya Umoja wa Mataifa  pia huweka kanzidata ya uhamiaji duniani.[4] Maendeleo ya hivi Karibuni katika utafiti wa uhamiaji kupitia mtandao unawezesha kuelewa vizuri zaidi mwelekeo wa uhamiaji na nia za uhamiaji .[5][6]

Kiwango kikubwa cha uhamiaji hufanyika katika nchi za kaskazini na nchi za kusini. Wahamiaji wengi kutoka nchi zilizoendelea huhama kuenda nchi zilizoendelea zaidi na takriban 43% ya wahamiaji kutoka nchi zinazoendelea huhama kuenda nchi zingine zinazoendelea. Hazina ya Umoja wa Mataifa kuhusu Idadi ya Watu ilitoa ripoti kwamba nchi za kaskazini zilipata ongezeko kubwa zaidi la wahamiaji tangu mwaka 2000 (milioni 32) ikilinganishwa na nchi za Kusini (milioni 25), nchi za kusini zilipata ukuaji wa kiwango kikubwa zaidi. Kati ya mwaka 2000 na mwaka 2013 wastani wa kiwango cha mabadiliko ya idadi ya wahamiaji katika nchi zilizoendelea (2.3%) ilizidi kidogo ile ya nchi zinazoendelea (2.1%).

Marejeo

  1. "Migrations country wise". Iliwekwa mnamo 7 June 2014.  Check date values in: |accessdate= (help). One of the major migration rushes took place in the gold run in 19th century in California, Australia, and Africa.
  2. Kigezo:WebbrefSV
  3. http://siteresources.worldbank.org/INTLAC/Resources/Factbook2011-Ebook.pdf
  4. http://esa.un.org/unmigration/wallchart2013.htm
  5. Oiarzabal, P. J.; Reips, U.-D. (2012). "Migration and diaspora in the age of information and communication technologies". Journal of Ethnic and Migration Studies 38 (9): 1333–1338. doi:10.1080/1369183X.2012.698202. 
  6. Reips, U.-D., & Buffardi, L. (2012). Studying migrants with the help of the Internet: Methods from psychology, Journal of Ethnic and Migration Studies, 38(9), 1405–1424. doi:10.1080/1369183X.2012.698208 http://www.uni-konstanz.de/iscience/reips/pubs/papers/2012ReipsBuffardi_JEMS.pdf