Nenda kwa yaliyomo

Maadili ya utafiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Maadili ya utafiti yanahusu msingi wa kanuni za kimaadili kwa mada mbalimbali yanayohusiana na utafiti wa kisayansi, hivyo matumizi ya kanuni adilifu katika mada mbalimbali zinazohusu binadamu. Hizi ni pamoja na kubuni na kutekeleza utafiti juu ya binadamu na wanyama, nyanja mbalimbali za kashfa za kielimu pamoja na makosa ya kisayansi (kama udanganyifu, upotoshaji wa data na wizi (kunakili na kutangaza kazi za wengine), kujulisha makosa; udhibiti wa utafiti, nk.

Maadili ya utafiti yaliendelea pakubwa kama dhana katika utafiti wa tiba. Mkataba muhimu hapa ni Tamko la 1974 la Helsinki. Nurenberg Code ni mkataba wa awali, lakini bado una mipasho ya maana. Utafiti katika sayansi ya jamii unawakilisha masuala kadhaa tofauti na yale ya utafiti wa matibabu.

Nyanja ya utafiti wote wa kisayansi umejengwa kwenye msingi wa uaminifu. Wanasayansi huwa na imani kuwa matokeo yaliyoripotiwa na wengine ni halali. Jamii huamini kwamba matokeo ya utafiti huonyesha jaribio lenye uaminifu la wanasayansi kueleza dunia kwa usahihi na bila upendeleo. Lakini uaminifu huu utaendelea tu kama jamii ya kisayansi itajitolea yenyewe kueneza maadili ya kisayansi yanayohusiana na vitendo vya kimaadili. [1]

Kuna masuala mengi ya kimaadili ambayo yanafaa yatiliwe maanani kwa utafiti. Wasomi wa jamii wanahitaji kufahamu kuwa wana jukumu la kulinda usalama wa kupatiana ruhusa halisi na kujua malengo ya wale wote wanaoshiriki katika utafiti. Hawapaswi kutumia vibaya taarifa wanazopata, na kunafaa kuwe na jukumu la kimaadili fulani linalofaa kuchukuliwa kwa washiriki. Kuna wajibu wa kulinda haki za watu katika masomo hayo na vilevile siri na usikivu. Usiri wa wale wanaohusika katika uchunguzi lazima ufanyike, kuweka siri zao na kutokujulikana salama. Kama inavyodokezwa katika BSA for Sociology, maadili haya yote lazima yaheshimiwe isipokuwa kama kuna sababu nyingine kuu za kutofanya hivyo - kwa mfano, shughuli za kigaidi au zilizopigwa marufuku.

Maadili ya utafiti katika muktadha wa matibabu yamejaa principalism, mbinu ambayo imekosolewa kuwa nje ya muktadha. [2]

Masuala muhimu

[hariri | hariri chanzo]

Matokeo ya utafiti katika machapisho, idadi ya masuala muhimu ni pamoja na: [3]

  • Uaminifu. Uaminifu na uadilifu ni wajibu wa kila mwandishi na mtu, mtaalam na mwanachama wa bodi la kuhariri.
  • Mchakato wa Mapitio. Mapitio ya mchakato huchangia kudhibiti ubora na ni hatua muhimu kujua uhalali wa utafiti [4]
  • Viwango vya kimaadili. Majarida ya karibuni ya tahariri yaliashiria uzoefu wa shughuli zisizofaa. [5] [6]
  • Uandishi. Nani anaweza kudai haki ya uandishi? [3] Ni mpangilio upi unafaa waandishi kutajwa?
  1. National Academy of Sciences. 2009. On Being a Scientist: Toleo la Tatu. Washington, DC: The national Academies Press. Kinapatikana: http://www.nap.edu/catalog.php?record_id=12192.
  2. Shaw SE, Petchey RP, Chapman J, Abbott S (2009). " upanga unaokata kuwili? Utafiti wa afya na sheria za utafiti katika huduma za msingi,UK. " Social Science & Medicine, 68: 912-918
  3. 3.0 3.1 Hubert Chanson (2008). Digital Publishing, Ethics and Hydraulic Engineering: The Elusive or "Boring" Bore?. In: Stefano Pagliara 2nd International Junior Researcher and Engineer Workshop on Hydraulic Structures (IJREW'08), Pisa, Italy, Keynote, pp. 3-13, 30 Julai-1 Agosti 2008. ISBN 978-88-8492-568-8. {{cite book}}: External link in |title= (help)
  4. Hubert Chanson (2007). Research Quality, Publications and Impact in Civil Engineering into the 21st Century. Publish or Perish, Commercial versus Open Access, Internet versus Libraries ?. Canadian Journal of Civil Engineering, NRC, Vol. 34, No. 8, pp. 946-951 (DOI:10.1169/L07-027). {{cite book}}: External link in |title= (help)
  5. D. Mavinic (2006). The "Art" of Plagiarism. Canadian Journal of Civil Engineering, NRC, Vol. 33, Iss. 3, pp. iii-vi.
  6. AIAA (2007). Publication Ethical Standards: Guidelines and Procedures. AIAA Jl, Vol. 45, No. 8, Editorial, No. 8, p. 1794 (DOI: 10.2514/1.32639). {{cite book}}: line feed character in |publisher= at position 25 (help); line feed character in |title= at position 31 (help)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Maadili ya utafiti kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.