Nenda kwa yaliyomo

Lord Tariq na Peter Gunz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lord Tariq & Peter Gunz

Maelezo ya awali
Asili yake The Bronx, New York
Aina ya muziki Hip hop
Miaka ya kazi 1996 - 1999
Studio Columbia Records
Ame/Wameshirikiana na Shaquille O'Neal
Wanachama wa zamani
Lord Tariq
Peter Gunz

Lord Tariq na Peter Gunz lilikuwa kundi la marapa wawili kutoka nchini Marekani, ambao ni Sean "Lord Tariq" Hamilton na Peter "Peter Gunz" Pankey. Mnamo mwaka wa 1996 washkaji hao walipata kuuza sura katika albamu ya Six ya kundi la Whodini katika wimbo wao wa "Can't Get Enough", na pia wakawasaidia kuandika nyimbo zingine mbili za katika albamu hiyo.

Kunako mwaka wa 1998, walipata kutoa single zao mbili na kubahatika kuingiza moja katika platinamu - "Deja Vu (Uptown Baby)" kibao ambacho kilishika nafasi ya 9 katika chati za Billboard Hot 100 Bora na kibao kilitoka katika albamu yao moja tu ya Make It Reign.

Albamu hiyo ilishirikisha marapa wakubwa kabisa kama vile Big Pun, Fat Joe, Sticky Fingaz, Kurupt na Cam'ron. Lakini kundi halikutoa kibao kingine tangu hapo na badala yake wakatawanyika baada ya muda mfupi. Mtoto wa Peter Gunz, Cory Gunz naye pia ni rapa.

Lord Tariq ana albamu ya kujitegemea iitwayo The Barcode, ambayo imemshirikisha Peter Gunz na mtoto wake Cory Gunz. Lord Tariq pia alishawahi kushirikiana na Jay-Z na Shaquille O'Neal mnamo mwaka wa 1998 katika wimbo uitwao "Analyze This". Remix ya wimbo huo baadaye iliondolewa mistari ya Shaq's na badala yake ikawekwa ya Nas.

Maelezo ya Albamu
Make It Reign
  • Imetolewa tar: 2 Juni 1998
  • Nafasi iliyoshika: #38 US, #8 Top Hip Hop/R&B
  • Mwisho wa Tunu za RIAA: Platinam
  • Single: "Deja Vu (Uptown Baby)", "We Will Ball"
  • Whitburn, Joel (2002). Top Pop Singles, 1955-2002. Menomonee Falls, Wisconsin: Record Research. ISBN 0-89820-155-1. {{cite book}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lord Tariq na Peter Gunz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.