Lauren Williams (mwandishi wa habari)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lauren Williams (mwandishi wa habari)
Lauren_Williams mnamo 2015
Lauren_Williams mnamo 2015
Nchi Marekani
Kazi yake mwandishi wa habari

Lauren Williams ni mwandishi wa habari wa Marekani.

Alianza kufanya kazi na jarida la The Root kama mhariri mshirika mwaka 2010[1] akapandishwa kuwa naibu mhariri mwezi mnamo Disemba mwaka 2011 na kufanya kazi kwenye kitengo hicho kwa miaka miwili na miezi mitano.[1]

Baadaye akafanya kazi kama mhariri wa habari akiwa na jarida la Mother Jones kabla ya kuajiriwa kwenye tovuti ya Vox.[1] Williams alianza kufanya kazi na Vox kama mhariri msimamizi mwaka 2014 miezi miwili baada ya kuzinduliwa.[2] Akawa mhariri mtendaji mwaka 2017 na miezi tisa baadae alipandishwa mpaka kuwa mhariri mkuu,[3] akichukua nafasi ya Ezra Klein, na pia akabeba majukumu ya Makamu wa rais.[4][5] wakati wa umiliki wake alisimamia biashara zote za Vox.com pamoja na vitengo vyote vya uhariri, kituo cha YouTube, madarasa yaliyopangwa, pamoja na programu za televisheni.[2] Aliacha kufanya kazi na shirika hilo mwaka 2021 kwa lengo lakuzindua shirika la habari lisilotengeneza faida la Watu Weusi lenye jina Capital B akishirikiana na Akoto Ofori-Atta.[2][6]

Williams ameolewa.[1]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 Dunn, Laura Emily (2017-03-31). "Women in Business Q&A: Lauren Williams, Executive Editor, Vox.com". HuffPost (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-02-18.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  2. 2.0 2.1 2.2 Spangler, Todd (2020-11-20). "Vox Co-Founder Ezra Klein Exiting for NY Times, Top Editor Lauren Williams Leaving to Launch Nonprofit". Variety. Iliwekwa mnamo 18 February 2021.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "Vox Promotes Lauren Williams to Executive Editor, Makes Additional Staffing Moves" (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2021-02-18. 
  4. Stelter, Brian (2017-09-26). "Lauren Williams named editor in chief of Vox; Ezra Klein to be editor at large". CNNMoney. Iliwekwa mnamo 2021-02-18. 
  5. Tracy, Marc. "Vox Finds Its Next Top Editor at The Atlantic", The New York Times, 2021-02-16. (en-US) 
  6. Fischer, Sara (2020-11-20). "Ezra Klein and Lauren Williams are leaving Vox". Axios (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-02-18.  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lauren Williams (mwandishi wa habari) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.