Kwabena

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwabena ni jina la kiume la Kiafrika miongoni mwa watu wa Akan (kama vile Ashanti, Akuapem, Akyem, Fante) nchini Ghana lenye maana ya "kuzaliwa siku ya Jumanne" katika lugha ya Akan, kulingana na mfumo wao wa kutaja siku. Watu wanaozaliwa siku fulani wanatarajiwa kuonyesha tabia au sifa na Utamaduni zinazohusiana na siku hizo.[1][2]

Kwabena ana jina la utambulisho "Ogyam" au "Ebo" lenye maana ya urafiki. [3][4][5] Hivyo, wanaume wanaoitwa Kwabena wanatarajiwa kuwa wapole na wenye urafiki.[6]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kwabena kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.