Nenda kwa yaliyomo

Kuzingirwa kwa Amida

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kuta za ngome ya Amida.

Kuzingirwa kwa Amida lilikuwa shambulio la kijeshi dhidi ya mji wa Amida (leo Diyarbakır, Uturuki) ulioko mpakani mwa Dola la Roma na Dola la Wasasani. Lilifanyika mwaka 359 BK ambapo jeshi la Wasasani chini ya mfalme Shapur II lilivamia Dola la Roma Mashariki. Shapur alitaka kutumia kutokuwepo kwa Kaisari wa Kirumi Constantius II ambaye alikuwa anashughulikia mambo katika sehemu ya magharibi ya Dola.

Mji wa Amida ulitekwa, lakini faida kimkakati ilikuwa ndogo. Ammianus Marcellinus, afisa wa jeshi la Kirumi, alitoa maelezo makini ya kuzingirwa huko katika kazi yake (Res Gestae). Ammianus alihudumu chini ya Ursicinus, Magister Equitum (mkuu wa farasi) wa Mashariki, wakati wa matukio ya kuzingirwa.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. John Harrel, Nisibis War, p. 148.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kuzingirwa kwa Amida kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.