Kupima ubikira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kupima Ubikira)

Kupima ubikira ni zoezi na mchakato wa ukaguzi wa viungo vya uzazi ya wasichana na wanawake ili kubainisha ikiwa wao hawajafanya mapenzi. Ina msingi katika dhana ya uongo kwamba kizinda cha mwanamke inaweza kuharibiwa kama matokeo ya ngono tu.

Kupima ubikira ni zoezi tata sana, hasa kwa sababu ya madhara yake kwa wasichana waliopimwa na kwa sababu si lazima matokeo yawe sahihi. Kunachukuliwa na Amnesty International kama ukiukaji wa haki za binadamu[1] na kumepigwa marufuku katika nchi nyingi.

Sababu za kupima[hariri | hariri chanzo]

Kulingana na AVERT, shirika la msaada la VVU na UKIMWI, kulikuwa na wastani wa watu milioni 22 wanaoishi na VVU katika Afrika kusini kwa Sahara mwishoni mwa 2007. Kusambaa kwa [2]VVU/ UKIMWI kumefanya ni muhimu kwa watu kutafuta njia ya kujilinda wao wenyewe na jamii zao. Chifu Naboth Makoni wa Zimbabwe, kiongozi wa watu wake, amechukua kulazimisha kupima ubikira kama njia ya kuwalinda dhidi ya VVU. Alisema mwaka 2004 kwamba analenga wasichana kwa sababu ni rahisi kuwadhibiti kuliko wavulana. [3] Katika Afrika ya Kusini, ambapo kupima ubikira ni marufuku, kabila la Wazulu linaamini kwamba zoezi hili huzuia kuenea kwa VVU na mimba za utotoni. [4] Mwanamke aliyehojiwa na Washington Post alisema kuwa "[kupima ubikira] ni muhimu ili wasichana wadogo wawe na hofu ya wavulana. Kwani kinachoendelea ni mvulana anakunyang'anya ubikira wako kwanza, na kitu unachojua haatimaye ni kuwa wewe ni mjamzito na una VVU. [4]

Mchakato wa kupima[hariri | hariri chanzo]

Mchakato wa kupima ubikira ni tofauti kulingana na kanda. Katika maeneo ambapo kupata madaktari ni rahisi, kama vile Uturuki kabla ya nchi kupiga marufuku zoezi hili, kupimwa mara nyingi kulifanyika katika ofisi ya daktari. [1] Hata hivyo, katika nchi ambapo madaktari hawapatikani, wapamaji mara nyingi huwa ni wanawake wazee walioheshimika au mtu yeyote anayeweza kuaminiwa kutafuta hymen. [4] Hii ni kawaida kati ya makabila ya Kiafrika ambayo hufanya zoezi hili.

Kutegemeana kama msichana anayepimwa ametangaza ni bikira, matokeo ya mtihani huu yananaweza kuwa furaha au hasira. Katika utamaduni wa Kizulu, kuna mila ambayo wasichana wa umri fulani wanaweza kucheza ngoma kwa mfalme. Hata hivyo, wanawali tu ndio wanaoruhusiwa kushiriki. [4] Kama ni msichana amepimwa na kutangazwa bikira, yeye huleta heshima kwa familia yake. Kama ni msichana amepatikana si bikira, baba yake huenda kulipa faini kwa 'kuchafua' jamii na msichana anaweza kutengwa kutoka kwa mabikira 'waliothibitishwa'. [5] Kwa sababu ambayo matokeo ya kuchukuliwa mchafu huwa kwa wasichana na familia zao, kupima ubikira kuna uwezo wa kuwa tukio la kubadilisha maisha.

Ubishi[hariri | hariri chanzo]

Wasiwasi mkuu wa maafisa wa afya kuhusu upimaji wa ubikira ni kwamba si njia sahihi ya kuamua ubikira. Kwa ujumla, mwanamke au msichana huchukuliwa bikira ikiwa hymen yake haijaharibiwa. Walakini, hymen ya mwanamke inaweza kuvunjwa au kuharibiwa na Masturbation na pia baadhi ya shughuli zisizo za kimapezi, ambazo ni pamoja uendeshaji wa farasi, gymnastics na kazi ya kutumia nguvu. Aidha, kama maumbile mengi ya mwili, mwonekano wa asili wa hymen unatofautiana katika mtu mmoja kwa mwingine, ni hata inawezekana kwa mwanamke kuzaliwa bila hymen. Hivyo, ukosefu wa hymen siyo lazima ni kiashirio kwamba mwanamke si bikira. [6][6][3]

Wapinzani wa zoezi la kupima ubikira huliita ukiukaji wa haki za binadamu. Kwa mfano, Amnesty International waliorodhesha kupima ubikira kama aina ya unyanyasaji dhidi ya wanawake. [1] makala hayo pia yalisema kuwa zaidi ya 90% ya madaktari 118 waliohojiwa katika utafiti wa 1999 walisema kuwa upimaji wa ubikira ulikuwa na mateso ya kisaikolojia kwa wagonjwa. Zaidi ya 50% ya madaktari hawa pia walieleza mingi ya mitihani hii hayakutolewa na mgonjwa wa ridhaa na makubaliano. [1]

Pia kuna wasiwasi juu ya usafi wakati wa kupima ubikira. Mwanaanthropolojia aliyehudhuria tukio la kupima ubikira katika Durban, Afrika ya Kusini aligundua kwamba mmoja wa wapimaji alitumia jozi ya kinga moja kwa wasichana wote 85. [5] Kwa sababu magonjwa mengi yanaweza kuenezwa kwa kupitisha ya maji ya mwili kwa njia hii, vipimo hivi vinaweza kuwa na hatari kwa wasichana wanaovipitia

Kupima ubikira ni marufuku katika nchi kadhaa. Hata hivyo, marufuku hizo, kama vile katika Afrika ya Kusini, mara nyingi huvunjwa. [4] Kupima ubikira kulipigwa marufuku nchini Uturuki mwaka 1999, baada ya wasichana watano waliotishiwa kupimwa kujaribu kujiua. [1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 Amnesty International. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-12-09. Iliwekwa mnamo 2010-01-26.
  2. AVERT, ilisomwa 13 Mei 2009
  3. 3.0 3.1 Kupima ubikira na VVU Kabla ya Ndoa, kutoka Habari Kutoka Afrika, Archived 2 Machi 2007 at the Wayback Machine. kupima ubikira na VVU Kabla ya Ndoa, kutoka Taarifa Kutoka Afrika. ilisomwa 4 Machi 2009.
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 The Washington Post ilisomwa 4 Machi 2009
  5. 5.0 5.1 LeClerc-Madlala, Suzanne (2001). "Virginity Testing: Managing Sexuality in a Maturing HIV/AIDS Epidemic". Medical Anthropology Quarterly 15 (4): 533–552. 
  6. 6.0 6.1 Chuo Kikuu cha California katika Santa Barbara SexInfo - The Hymen, Archived 11 Machi 2012 at the Wayback Machine. ilisomwa 4 Machi 2009. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "sexinfo" defined multiple times with different content