Kizuizi cha ACE
Captopril, the first ACE inhibitor | |
Data ya kikliniki | |
AHFS/Drugs.com | Drug Classes |
Kategoria ya ujauzito | ? |
Hali ya kisheria | ? |
Vitambulisho | |
Nambari ya ATC | ? |
Data ya kikemikali | |
Fomyula | ? |
Vizuizi vya kimeng'enya cha kubadilisha Angiotensin (vizuizi vya ACE) ni kundi la dawa zinazotumiwa hasa kwa shinikizo la juu la damu, kushindwa kwa moyo, ugonjwa wa figo na ugonjwa wa moyo.[1] Matumizi mengine yanaweza kujumuisha kipandauso na ugumu wa ngozi (scleroderma).[2] Kawaida huchukuliwa kwa mdomo, ingawa zingine zinapatikana kwa sindano.[1][3]
Vizuizi vya ACE kwa ujumla huvumiliwa vizuri.[4] Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kikohozi, kizunguzungu, shinikizo la chini la damu, kupungua kwa utendaji wa figo na potasiamu nyingi.[3] Kupungua kwa utendakazi wa figo hutokea kwa watu walio na mtiririko mdogo wa damu kwenda kwenye figo (renal artery stenosis).[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha uvimbe wa ndani wa ngozi na tishu za chini ya ngozi (angioedema).[1] Zinaepukwa ikiwa kuna matatizo makubwa ya figo au historia ya angioedema.[4] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[3] Dawa hii hufanya kazi kwa kusimamisha kimeng'enya cha kubadilisha angiotensin na hivyo basi kupunguza angiotensin II.[2] Viwango vya chini vya angiotensin II husababisha upanuzi wa mishipa ya damu na kuongezeka kwa kutolewa kwa maji na sodiamu na figo.[1] Uchunguzi wa damu ili kuangalia utendaji wa figo kawaida hufanywa wiki moja baada ya kuanza kwa kizuizi cha ACE au baada ya kubadilisha dozi ya dawa.[4]
Vizuizi vya ACE, haswa captopril, vilianza kutumika katika matibabu mnamo mwaka wa 1981.[5] Zilitumika kwa kawaida kufikia mwaka wa 2021.[3] Nchini Marekani, ni matibabu ya mstari wa kwanza kwa shinikizo la juu la damu, pamoja na vizuizi vya njia ya kalsiamu, diuretiki ya thiazide, na vizuizi vya vipokezi vya angiotensin.[6] Nyingi zake zinapatikana kama dawa za kawaida na sio ghali sana.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 Hitchings, Andrew; Lonsdale, Dagan; Burrage, Daniel; Baker, Emma (2019). The Top 100 Drugs: Clinical Pharmacology and Practical Prescribing (kwa Kiingereza) (tol. la 2nd). Elsevier. ku. 50–51. ISBN 978-0-7020-7442-4. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-05-22. Iliwekwa mnamo 2021-11-09.
- ↑ 2.0 2.1 "List of ACE inhibitors + Uses, Types & Side Effects". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Aprili 2021. Iliwekwa mnamo 18 Aprili 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 Goyal, A; Cusick, AS; Thielemier, B (Januari 2021). "ACE Inhibitors". StatPearls. PMID 28613646.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 4.0 4.1 4.2 Haslam, Sally J. (2022). "8c. Renal impairment". Katika Courtenay, Molly; Griffiths, Matthew (whr.). Independent and Supplementary Prescribing: An Essential Guide (kwa Kiingereza) (tol. la Third). Cambridge: Cambridge University Press. uk. 146. ISBN 978-1-108-92851-9. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-01-17. Iliwekwa mnamo 2022-01-17.
- ↑ Sciences, International Relations Office
Faculty of Health and Medical (7 Agosti 2012). "Discovery of the ACE-Inhibitor Captopril". studies.ku.dk (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Septemba 2017. Iliwekwa mnamo 18 Aprili 2021.{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Herman, LL; Padala, SA; Annamaraju, P; Bashir, K (Januari 2021). "Angiotensin Converting Enzyme Inhibitors (ACEI)". StatPearls. PMID 28613705.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)