Kisoo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kisoo (lugha))

Kisoo ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Uganda inayozungumzwa na Wasoo. Mwaka wa 2002 idadi ya Wasoo imehesabiwa kuwa watu 21,534 lakini idadi ya wasemaji ni wachache zaidi kwa vile ni wazee tu ambao wamebaki kuizungumza lugha hiyo; Wasoo wengi wamebadili lugha na kuongea Kikaramojong kama lugha yao. Kwa hiyo inawezekana kuwa Kisoo itatoweka hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kisoo iko katika kundi la Kikuliak ambalo ni tofauti sana na lugha nyingine za Kinilo-Sahara.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kisoo kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.