Kisaho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kisaho ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Eritrea na Ethiopia inayozungumzwa na makabila wahamahamaji mbalimbali kama Waasa'orta, Wahadu na Waminiferi. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kisaho nchini Eritrea imehesabiwa kuwa watu 191,000. Pia kuna wasemaji 32,800 nchini Ethiopia (2007). Nchini Ethiopia Kisaho huzungumzwa na kabila la Wairob ambao si wahamahamaji. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kisaho iko katika kundi la Kikushi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kisaho kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.