Kiomotik

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kiomotik ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Kenya inayozungumzwa na Waomotik. Mwaka wa 1980 idadi ya wasemaji wa Kiomotik imehesabiwa kuwa watu 50 tu. Mwaka wa 2000 idadi ya kabila la Waomotik imehesabiwa kuwa watu 200 lakini wengi wao waliongea Kimaasai badala ya lugha yao ya Kiomotik. Kwa hiyo inaonekana kama lugha ya Kiomotik imekaribia kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiomotik iko katika kundi la Kinilotiki.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiomotik kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.