Nenda kwa yaliyomo

Kimlabri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kimlabri ni lugha ya Kiaustro-Asiatiki nchini Laos na Uthai inayozungumzwa na Wamlabri. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kimlabri nchini Uthai imehesabiwa kuwa watu 130 tu. Idadi ya wasemaji nchini Laos hata ni ndogo zaidi; mwaka wa 1982 kulikuwa na watu 24 tu. Maana yake, lugha ya Kimlabri imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimlabri iko katika kundi la Kikhmuiki.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kimlabri kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.