Nenda kwa yaliyomo

Kimbunga vumbi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kimbunga vumbi katika jangwa la Mojave.

Kimbunga vumbi (kutoka Kiing.Dust devil) ni dhoruba dogo la vumbi linalotokea wakati wa hali ya joto kali na hewa kavu. Mara nyingi hutokea katika maeneo ya jangwa au sehemu zilizo na mchanga mkavu au udongo laini ambao unaweza kunyanyuka kirahisi. Katika kufanikisha zoezi hili, hewa ya moto juu ya uso wa ardhi inapopanda juu kwa haraka, inasukuma hewa ya baridi kushuka chini. Mzunguko huu wa hewa unaweza kusababisha kimbunga kidogo ambacho huchota vumbi na mchanga na kuunda mviringo kwa kasi.

Kimbunga vumbi huko Kihonda, Morogoro, Tanzania.

Utofauti wake na na vimbunga vikubwa kama vile tufani, kimbunga cha hakina nguvu kubwa za kuharibu vitu au hata kudumu kwa muda mrefu. Kasi na mzunguko wake huisha ndani ya muda mfupi. KImsingi huwa hakina athari kubwa kwa mazingira, lakini kinaweza kunyanyua vitu vidogo na vumbi kwa muda mfupi.


Ukiachana na kimbunga hiki, pia kuna majina mengine ya kimbunga cha aina hii katika maeneo tofauti. Kwa mfano, nchini Australia kinajulikana kama "willy-willy," wakati nchini Marekani kinaitwa "dust whirl" au mara nyingine tu "whirlwind." Pia, kuna matukio yanayofanana ambayo yanaweza kutokea kwenye maji, ambapo huitwa "waterspouts" au wakati mwingine kwenye barafu ambapo huitwa "snow devils." Vimbunga hivi vinafanana kwa kanuni ya jinsi hewa inavyopanda na kuzalisha mzunguko wa haraka.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: