Kimani wa Mbogo
Kimani wa Mbogo ni mtunzi wa mashairi nchini Kenya. Amechangia kuenezwa na kukuzwa kwa lugha ya Kiswahili katika janibu zote nchini Kenya na mataifa mengine kunakozungumzwa lugha hiyo.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Kimani wa Mbogo alizaliwa Kijijini Mbichi, katika wilaya ya Gatundu (wilaya ya Kiambu nyakati hizo), nchini Kenya, Kuliko sasa jimbo la Kiambu.
Alihudhuria shule ya msingi ya Gatei (1992-1999) na baadaye shule ya upili ya Mbichi (2000-2003), Gatundu Kaskazini, Kenya. Huko Mbichi ndiko kilichipuka kipawa chake cha utunzi na uandishi. Mara kwa mara alitunga mistari ambayo baadaye ingemwabirisha chombo cha utunzi na hatimaye kuwa malenga. Alijibidiisha kutunga na kutuma mashairi kwenye vyombo vya habari. Hata hivyo, mashairi yake hayakuchapishwa na hakuvunjika moyo kwa jambo hilo.
Utunzi wake ulikumbwa na matatizo si haba yakiwemo kukua kwenye mazingira ya watu wasioufahamu wala kuuthamini ufasaha wa Kiswahili na utunzi wa mashairi.
Alijiunga na vyuo vya uhasibu CEDAT mjini Thika (2004) na German Training Institute, Nakuru (2009) kwa somo la uhasibu na baadaye chuo kikuu cha Kenyatta kwa somo la Teknolojia.
Kimani alifunza Kiswahili na Kiingereza katika shule mbalimbali zikiwemo Vineyard Joy Academy (2005) na Gatei Joyland Academy (2006-2008) alikokuwa naibu wa mwalimu mkuu.
Kwa sasa, Kimani ni ofisa wa shirika moja lisilo la kiserikali jijini Nairobi, Kenya.
Aliomba dua tungo zake zichapiswe kutwa moja kwenye majarida, magazeti, vitabu na redioni, jambo ambalo limetimia kwa sasa licha ya kujaribu jambo hili kwa muda mrefu tangu alipokuwa mwanafunzi shuleni Mbichi. Kwa sasa amechangia kwenye redio (zikiwemo QFM, KBC na Sauti ya Amerika), majarida na magazeti mbalimbali (likiwema Taifa Leo)kwa utunzi na uandishi wake.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kimani wa Mbogo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |