Nenda kwa yaliyomo

Kilimanjaro Christian Medical Centre

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kilimanjaro Christian Medical Centre inapatikana kaskazini mwa mkoa wa Kilimanjaro imekaribiana na mlima Kilimanjaro. Ilifunguliwa machi 1971 na shirika la wasamaria ambao walipanga na kuchangisha michango ya kujenga na kununua vifaa mbalimbali vya matibabu. KCMC ni hospitali ya rufaa yenye uwezo wa kuhudumia zaidi ya watu milioni 15 kaskazini mwa Tanzania. Ni hospitali kubwa yenye uwezo wa kupokea wagonjwa 500-800, vitanda 630, wanafunzi 1852, wafanyakazi 1300 na wageni 1000.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]