Nenda kwa yaliyomo

Kili Paul

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kili Paul
AmezaliwaYusufu Paul Kimesera
9 Oktoba 1994 (1994-10-09) (umri 30)
UtaifaMtanzania
Asili yakeMmasai
UraiaMtanzania
ElimuDarasa La Saba
Kazi yakeMraghibishi (Influencer)
Anajulikana kwa ajili yaKuimba na Kucheza nyimbo za Kihindi
MtindoMavazi ya Kimasaai
NyumbaniLugoba, Kibaha
DiniMkristo
NdoaHana
NduguNeema Paul

Yusufu Paul Kimesera (amezaliwa 9 Oktoba 1994 (1994-10-09) (umri 30) anafahamika kwa jina lake la mtandaoni kama Kill Paul. Ni Mmasai maarufu kutoka nchini Tanzania. Anasifika zaidi kwa kucheza nyimbo za Kihindi. Amejizolea mashabiki wengi kutoka bara Asia. Hasa India. Huonyesha kipawa chake katika mitandao ya Kijamii hasa Tiktok na Instagram.[1]

Maisha yake

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa katika kijiji cha Mindu Tulieni katika mji wa Lugoba uliopo Mkoani Pwani nchini Tanzania. Wazazi wake wote wawili ni wamasai wanao jishughurisha na shughuri ya ufugaji. Kabla ya kuwa maarufu kwenye mitandao ya kijamii kupitia maudhui yake yenye kuhusisha nyimbo na miziki ya kihindi, Kili Paul alijihusisha zaidi na uandaaji wa Maudhui yenye kuelezea maisha ya kila siku ya masai na tamaduni zao. Maudhui haya yalipendwa na wengi na mara kadhaa alikuwa akiimba na kucheza nyimbo za aina tofauti tofauti na taratibu mwaka 2021 yeye pamoja na dada yake afahamikaye kama Neema Paul akaanza kupata wafuasi wengi wenye kupendelea kila akipandisha maudhui yenye kuhusisha nyimbo za kihindi na ni hapo ndipo alipo amua kuwekeza muda mwingi katika maudhui za aina hiyo.

Mmoja ya watu maarufu walio na wanao pendezwa na maudhui za kili paul na dada yake ni Waziri mkuu wa India anaye fahamika kwa jina la Narendra Modi[2].

  1. Mtengeneza Maudhui bora (2022) - TDA[3]
  1. "Kili Paul and Neema: A show of the power of social media". The Citizen (kwa Kiingereza). 2022-01-02. Iliwekwa mnamo 2024-05-26.
  2. Ridhi Suri, India TV News (2022-03-01). "Tanzanian sensation Kili Paul's 'mind-blown' after PM Modi gives shoutout on Mann ki Baat". www.indiatvnews.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-05-26.
  3. KWAYU-SERENGETI BYTES. "Tanzania Digital Awards". Tanzania Digital Awards (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2024-05-26.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kili Paul kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.