Kikokoteo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kikokoteo cha wanafunzi wa shule(Pickett N902-T simplex trig)
Mstari wa kusukumwa juu ya kikokoteo ulisaidia kulinganisha namba za rula zake

Kikokoteo ni rula yenye kikokoto iliyotumika kama nyenzo ya kufanya hisabati hususani katika kuzidisha na kugawanya na kutafuta vipeo na vipeuokabla ya ujio na uendelezaji wa matumizi makubwa ya Vikokoteo vya kielektroniki kuanzia mwaka 1974 [1] Rula hizi zilitengenezwa kwa maumbo na vipimo anuwai kutegemeana na fani husika kama vile kutumika katika hisabati, uhasibu, uongozaji wa ndege, uhandisi n.k

Kikokoteo kilivumbuliwa na William Oughtred na wenzake katika karne ya 17 kutokana na kazi za hisabati za John Napier.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Maor, Eli (2009). e: The Story of a Number. Princeton University Press. p. 16. ISBN 978-0-691-14134-3. "Then in the early 1970s the first electronic hand-held calculators appeared on the market, and within ten years the slide rule was obsolete