Kikacipo-Balesi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kikacipo-Balesi ni lugha ya Kinilo-Sahara inayozungumzwa na makabila matatu, yaani Wakacipo nchini Sudan Kusini na Wazilmamu na Wabaale nchini Ethiopia. Idadi ya wasemaji wa Kikacipo-Balesi imehesabiwa kuwa watu 9120, yaani 5000 nchini Sudan Kusini (2010) na 4120 nchini Ethiopia (2000). Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kikacipo-Balesi iko katika kundi la Kisurmi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kikacipo-Balesi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.