Nenda kwa yaliyomo

Kifo cha Abdul Wali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Abdul Wali alikuwa mkulima kutoka Afghanistan aliyefariki mikononi mwa majeshi ya Marekani mnamo tarehe 21 Juni, 2003, akiwa na umri wa miaka 28. Tukio la kifo chake lilitokea akiwa ameshikiliwa kwa takribani siku tatu katika kambi ya Marekani iliyokuwepo mile 10 (km 16) kusini mwa mji wa Asadabad, katika mko wa Kunar, Afghanistan. Alishikiliwa kwa tuhuma za mchongo za kuhusika katika shambulizi la roketi katika kambi hiyo hiyo. Kadhia ya mateso kwake ilitukia baada ya kujisalimisha kwa hiari. Gavana wa eneo hilo, Ndugu Said Akbar, alimshauri Wali ajisalimishe ili aondolewe tuhuma dhidi yake.[1]

Sababu ya kifo chake awali iliripotiwa kuwa mshituko wa moyo. Suala hili likachukua sura mpya baada ya maafisa watatu kutoka kitengo cha jeshi la kutoa ushahidi kwamba mamluki wa CIA David Passaro alimshambulia Wali. Passaro, aliyekuwa mtangulizi wa Jeshi la nchi Kavu la US, alishutumiwa kumpiga Wali nyakati za usiku kwa siku mbili mfululizo. Hali iliyosababisha majeraha makubwa ikiwa ni pamoja na kuvunjika kwa mfupa wa nyonga. Waendesha mashtaka walisema ya kwamba Passaro aliagiza wanajeshi wasiruhusu kupata usingizi kwa Wali. Hakupaswa kulala wala kunywa, achilia mbali kupata riziki ya chakula. Hata maji hakuna. Kama haitoshi, walimwingia mwilini kwa vipigo visivyo na hesabu. Miongoni mwa majeraha mengine, Wali alihisiwa kuwa amevunjika nyonga. Hivyo basi suala la kupata mkoko likawa kipengele.

Mashahidi walieleza kwamba katika kikao kimoja Passaro, akiwa na viatu vya kijeshi, alimkanyaga Wali kwenye sehemu za siri kwa nguvu. Kisha akamuinua angani na kumtupa chini. Alimpiga kwa mikono na miguu kwa kutumia tochi nzito. Kwa nguvu akaikandamiza tochi kwenye tumbo la Wali.[2][3] Baada ya usiku wa pili wa kipigo, Wali aliomba wanajeshi wamuuwe ili kuepuka mateso. Alilia kwa uchungu akisema "Ninakufa." Wali alifariki siku ya nne akiwa mikononi mwa jeshi la Marekani. [3]

Passaro alishtakiwa kwa makosa mawili, mosi la mashambulizi yenye lengo la kuleta maumivu na lingine la shambulizi lililosababisha majeraha makubwa. Katika kadhia hii, Passaro alikuwa na hatia inayopelekea hukumu hadi miaka 40 gerezani. Hata hivyo, Passaro alipatikana na hatia ya makosa moja ya mashambulizi yaliyosababisha majeraha makubwa, na makosa matatu madogo ya mashambulizi sahili. Hivyo Passaro alikkwenda gerezani kwa miaka 11.5.[4] Said Akbar aliandika kwa hakimu, akimuomba aweke adhabu kali zaidi, akisema kifo cha Wali kilisaidia waajiri wa kigaidi. Passaro alihukumiwa kifungo cha miaka 8 na miezi 4 gerezani na miaka mitatu ya uangalizi. Hii ilikuwa zaidi ya mara mbili ya yale ambayo miongozo ya hukumu ya shirikisho kawaida inapendekeza kwa mashtaka ya mashambulizi.[5]

Hakimu alimwambia Passaro kwamba alikuwa na bahati kubwa kwamba hakuna ripoti ya uchunguzi wa maiti, vinginevyo huenda angeshitakiwa kwa mauaji.[6] Mnamo mwaka wa 2010, adhabu ya Passaro ilipunguzwa hadi miaka 6 na miezi 8. Mahakama ya rufaa iliamua kwamba hakimu alishindwa kueleza kikamilifu mantiki yake kwa kupita miongozo. Passaro aliachiliwa kutoka gerezani tarehe 26 Januari, 2011.[1][7]

Wakati wa kesi ya Passaro, mkewe wa zamani, Kerry, alisema kwamba alimpiga na kumtesa kihisia wakati wa ndoa yao. Baadaye alisema kwa mwandishi kwamba hakuwa na mshangao na kile alichofanya Passaro.[8]

[1][3] Yeye ndiye mtu wa kwanza na wa pekee aliyehusishwa na CIA ambaye amehukumiwa katika kesi ya unyanyasaji baada ya Septemba 11.[9][10]

  1. 1.0 1.1 1.2 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named :0
  2. AFP. "Mahakama yathibitisha hukumu ya mkandarasi wa CIA kwa unyanyasaji wa wafungwa", August 12, 2009. 
  3. 3.0 3.1 3.2 Weigl, Andrea. "Passaro atahudumia miaka 8 kwa kipigo", February 14, 2007. 
  4. "Kesi ya Passaro - Makosa ya mashambulizi". Findlaw (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2022-04-16.
  5. "Mfanyakazi wa CIA alihukumiwa kwa unyanyasaji wa Afghan". Chicago Tribune. Agosti 18, 2006. Iliwekwa mnamo 2023-03-09.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Ex-CIA contractor jailed for beating detainee". NBC News (kwa Kiingereza). Februari 13, 2007. Iliwekwa mnamo 2022-03-30.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Office (USAO), U. S. Attorney's. "Ofisi ya Wakili wa Marekani - Wizara ya Haki". www.justice.gov (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-03-09.
  8. WRAL (2004-07-21). "Mke wa Passaro asema kuhusu udanganyifu, unyanyasaji". WRAL.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-04-16.
  9. Thompson, Estes. "Majuri waanza kujadili kesi ya mkandarasi wa zamani wa CIA anayeshutumiwa kwa kipigo cha mfungwa wa Afghan", SignOnSanDiego, August 16, 2006. 
  10. "CIA inakiri kuwa iliwachunguza wafanyakazi wa Seneti", The Guardian, July 31, 2014. 

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]


Makala hii ni sehemu ya mradi wa kuboresha Wikipedia na Wikamusi ya Kiswahili. Unaweza kusaidia kuihariri na kuongeza habari.