Kidampelas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kidampelas (pia Kidian) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wadampelas kwenye kisiwa cha Sulawesi. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kidampelas imehesabiwa kuwa watu 2000. Hata hivyo idadi ya Wadampelas ni 10,000 yaani Wadampelas wengi wameanza kuacha lugha yao na Kidampelas iko hatarini mwa kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidampelas iko katika kundi la Kicelebiki.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kidampelas kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.